Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, hayati Mhandisi Suleiman S. Suleiman.
SALAMU ZA RAMBIRAMBI
Dar es Salaam, 19 Januari, 2016
Uongozi na
wafanyakazi wa Fastjet Tanzania umepokea
kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha ghafla cha Mkurugenzi Mkuu wa wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania,
hayati Mhandisi Suleiman S. Suleiman.
Tunaungana
na familia, marafiki, ndugu, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) na Serikali ya
Jamhuri ya Muungano Tanzania kutuma salamu za rambirambi katika kipindi hiki
cha kuomboleza.
Fastjet
Tanzania imefanyakazi kwa ukaribu na Mhandisi Suleiman na tunatambua mchango
wake katika kukuza sekta ya usafiri wa anga nchini.
Tutaukosa
kwa kiwango kikubwa ushauri, uongozi na ushauri wake kutokana na kifo chake.
Tunaomba
roho yake ipumzike kwa amani peponi.
Amin.
Imetolewa na Meneja Mkuu wa fastjet
Tanzania, John Corse.
|
Post a Comment