Waandishi wa habari wakifuatilia kikao hicho. |
Baadhi ya waqkuu wa Idara mbalimbali katika halmashauri hiyo ya jiji la Mbeya wakifuatilia mkutano . |
Na Emanuel Madafa,Mbeya.
Halmashauri ya jiji la mbeya imeshindwa kufikia lengo lake la
ukusanyaji wa mapato kwa mwaka 2015-16 kutokana na mwitikio hafifu kwa wananchi
kuhusu ulipaji huo wa kodi tozo na ada mbalimbali za serikali.
Imesema kwa miaka miwili makusanyo bado hayalidhishi hivyo
kufanya halmashauri hiyo kushindwa kutoa huduma bora kwa wananchi wake hali ambayo imechangia kwa kiwango
kikubwa kuleta malalamiko kwa jamii.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya Kaimu
Mkurugenzi wa jiji hilo Dkt Samuel Lazaro amesema hadi kufikia novemba 30 mwaka huu walikuwa
wamekusanya asilimia 24 ya makisio
ukusanyaji wa mapato 2015 -16 ambapo
lengo ilikuwa ni kufikia asilimia 40 hadi 50.
Amesema asilimia hiyo ndogo ya ukusanyaji wa mapato lazima iendane na
asilimia ya utoaji wa huduma kwa wananchi wake hivyo wao kama halmashauri hawana sababu ya
kutupiwa lawama katika suala hilo.
Amesema wao kama halmashauri wanatakiwa kutoa huduma bora kwa
jamii yake lakini kutokana na mwitikio huo mdogo wa ulipaji wa kodi,ada na tozo
mbalim bali za serikali umechangia
kuwepo na malalamiko kwa jamii juu utoaji wa huduma bora hususani ,afya,miundombinu na huduma
nyinginezo.
Amesema wao kama halmashauri kupitia baraza la Madiwani
wamekusudia kutoa huduma bora kwa jamii sanjali na kuhakikisha kila mmoja
anatambua wajibu wake ambapo pia amewataka wananchi nao kutoa ushirikiano ili kuepuka
migongano hiyo .
Wakati huo huo mkurugenzi huyo amewatoa hofu wananchi juu ya
kukithiri kwa taka katika jiji hilo ambapo amedai kuwa halmashauri hiyo
imechukua hatua za haraka za ukodishaji wa magari matano ambayo yatahusika na
ukusanyaji wa taka katika maeneo mbalmbali ya jiji hilo ambayo tayari
yamekwisha anza kazi .
Mwisho.
Post a Comment