Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea wikiendi hii
kwa michezo saba kuchezwa katika viwanja tofauti, ikiwa katika mzunguko
wa 16 kwa kila timu kusaka pointi 3 muhimu katika raundi hiyo ya lala
salama.
Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam siku ya Jumamosi, Simba SC
watawakaribisha African Sports, JKT Ruvu watawakaribisha Majimaji FC
uwanja wa Karume, huku Mtibwa Sugar wakiwakaribisha Stand United kwenye
uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
Jijini Tanga, Wagosi wa Kaya Coastal Union watakua wenyeji wa Young
Africans uwanja wa Mkwakwani, Mwadui FC watakua wenyeji wa Toto Africans
uwanja wa Mwadui Complex, huku wakata miwa wa Kagera Sugar wakicheza
dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Ligi hiyo itaendelea siku ya Jumapili kwa mchezo mmoja ambapo
Maafande wa Mgambo Shooting watawakaribsiha Ndanda FC kwenye uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga.
Post a Comment