Wananchi wakiwa wanapanda Miti katika maeneo ya Mlima Mbeya(.Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira wakiwa wanabeba miti Tayari kwa kwenda kupanda.(.Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Bw Samweli Lazaro akiwa anapanda Mti.(.Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Mzee nae akuwa Nyuma kwenye zoezi la upandaji Miti |
Watumishi wa Almashauri ya Jiji wakiwa wapepunzika mara baada ya kumaliza kupanda Miti.(.Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Mkuu wa mkoa Mbeya ndugu Abbas Kandoro ameziagiza
halmashauri zote za wilaya katika mkoa wa mbeya na hifadhi za taifa zote
kuwaondoa watu wote waliovamia maeneo ya hifadhi za misitu pamoja na hifadhi ya
misitu mlima Mbeya, na wale wanaofanya shughuli za kibinadamu kando kando ya
mito kuacha kufanya hivyo mara moja ambapo ametoa siku 14 kwa halmashauri zote
kufanya tathmini na kutekeleza agizo hili.
Agizo lilitolewa katika hotuba iliyosomwa na mkuu wa wilaya ndg. Nyirembe Munasa ambae
alimuwakilisha mkuu wa mkoa katika uzinduzi wa wa kampeni ya upandaji miti hapo
jana ambapo kimkoa lilifanyika katika chanzo cha maji mto Imeta kilichopo kata ya Iganzo, ambapo jumla
ya miti elfu kumi na sita ilipandwa
ikiwemo miti ya kuhifadhi vyanzo vya maji elfu kumi na tano (15,000) na miti ya
kivuli na matunda elfu moja (1,000)
Katika hotuba hiyo Munasa aliwaasa wananchi kutunza miti
iliyokwisha pandwa kwa kuikinga na moto pamoja na kurudishia ile ambayo imekufa
na kwamba ni kazi bure kuendelea kupanda miti wakati ile iliyopandwa msimu uliopita ikiachwa bila matunzo hivyo
aliwataka wanachi pamoja na viongozi katika ngazi mbali mbali kufanya tathmini
ya miti iliyopandwa mwaka jana na kuhakikisha wanairudishia miti yote ambayo
imekufa na kuendelea kuitunza vema ile ambayo inaendelea vizuri
Hata hivo Munasa aliwasisitiza wananchi kudumisha mila,
desturi na tamaduni nzuri zinazolenga kuamsha ari ya upandaji, utunzaji miti na
kuchochea uendelezaji na uhifadhi wa mazingira yanayowazunguka ili kuleta
mabadiliko ya kimaendeleo na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi yaliyo
anza kuleta athari katika maeneo mengi na kwamba serikali imeweka lengo la
kupanda miti isiyopungua milioni moja na nusu kwa mwaka katika kila halmashauri
huku zoezi hilo likitarajiwa kukamilika na kufanyiwa tahtmini ifikapo mwezi
Juni,
Aidha alihitimisha hotuba kwa kuwataka wananchi kuyatunza
maziringa na kuhakikisha wanafuata sheria na taratizu zote zinazohusiana na
uhifadhi wa vyanzo vya maji na mazingira ambapo kauli mbiu mwaka huu ni “Panda Miti Kuhifadhi Vyanzo Vya Maji na
Mazingira,”
Post a Comment