Naibu Waziri Fedha na Mipango Dkt,Ashatu Kijaji akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Mbeya ( hawapo pichani) mara baada ya kufanya ziara katika Mpaka wa Tunduma na Zambia . |
Na Jamiimojablogu,Mbeya
Naibu waziri
wa fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji
ameitaka Mamlaka ya Mapato TRA Mkoa wa Mbeya kuhakikisha inaanda mpango maalumu
kwa ajili kudhibiti mapato yanayopotea kutokana na kushamili kwa biashara ya
ubadilishaji wa fedha kiholela katika mpaka wa Tunduma na Zambia.
Naibu waziri
huyo ametoa kauli hiyo Mkoani Mbeya mara baada ya kutembelea Mamlaka ya Mapato (TRA)
Mkoani humo na kutoa tathimini ya ziara yake aliyoifanya katika Mpaka wa
Tunduma na Zambia.
Amesema
serikali imekuwa ikipoteza mapato mengi hasa kutokana na kuwepo kwa biashara
hiyo kiholela pasipo serikali kupata mapato yake hivyo ameitaka mamlaka hiyo kuhakikisha inaweka
mpango kabambe utakao iwezesha serikali kupata mapato yake kutokana na biashara
hiyo.
Amesema
serikali lazima ijiendeshe yenyewe kwa kuongeza ukusanyaji wa mapato sanjali na
kuzuia mianya yote ya ukwepaji wa kodi pamoja na watu wote kuhakikisha wanalipa
kodi.
Amebainisha kuwa nchi inategemea mapato kwa ajili ya kutoa
huduma muhimu kwa wananchi na hivyo kuwaongezea wananchi matumaini kwa
kuwafikishia huduma muhimu.
Sehemu nyingine
ambayo ameiagiza mamlaka hiyo kuishughulikia mara moja ili serikali iweze kupata mapato yake ni
pamoja kuibuka kwa Saccos pamoja vikundi mbalimbali ambavyo vimekuwa
vikijihusisha na ukopeshaji wa fedha kwa liba kubwa hali ambayo pia imekuwa
ikiwapa mzigo mkubwa wananchi .
Katika hatua
nyingine Naibu waziri huyo ameuagiza
uongozi wa mamlaka ya mapato (TRA) Katika mpaka wa Tunduma na Zambia
kuhakikisha kuwa mizigo yote inayosafilishwa kupitia mpaka huo inafanyiwa
tathimini na kulipiwa kwa muda wa usio zidi siku moja tayari kuendelea na safari kwa inayoingia na
kutoka nje ya Tanzania.
Ziara ya Naibu Waziri
Dr. Kijaji ni ya kwanza Mkoani Mbeya tangu alipoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania tarehe 11 Desemba 2015 kushika wadhifa huo.
Mwisho.
Post a Comment