Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (katikati) akizungumza na Machifu wa kisukuma kwenye kituo cha Utamaduni Bujora, kulia pichani ni Jaji Mstaafu Mark Bomani na kushoto ni Chifu Charles Kafipa wa Bukumbi mkoani Mwanza


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amesimikwa uchifu wa kisukuma mara baada ya kutembelea kituo cha utamaduni wa kisukuma cha Bujora.

 Katika tuzo hiyo ya watemi wa kisukuma ambayo risala yake imeandikwa na kusainiwa na Katibu wa Umoja wa Watemi wa Kisukuma Mtemi CM. Dotto Itale, wamemtakia heri na kumuomba mwenyezi mungu amsaidie kufanya kazi zake vizuri na kumtunukia cheo cha Manju Mkuu kiongozi wa ngoma kubwa mwenye kughani umati wote ukaitikia, na kumpa jina la Sangija ambalo linaunganisha Mamanju wote.
BOFYA HAPA UTAZAME VIDEO YA KUSIMIKWA KWA MHE.NAPE 

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top