Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mwantumu Mahiza akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Bandari (TPA) mkoani Tanga jana wakati alipofanya ziara ya kuangalia utendaji wao na changamoto zinazowakabili. |
NA MWANDISHI WETU,TANGA.
IMEELEZWA kuwa agizo la Rais John Magufuli kusitisha safari za nje kwa
watendaji wa serikali nchini zimesababisha Bandari ya Tanga
kufanyakazi chini ya kiwango na kulazimika kukodi vifaa kwa gharama
kubwa nje ya nchi.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Meneja wa bandari ya Tanga,Henry Arika
wakati mkuu wa Mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza alipofanya ziara ya siku
mmoja kukagua shughuli zinazofanywa na bandari hiyo.
Alisema kuwa hatua hiyo ya kusitishwa kwa safari mpaka vibali
imechangia bandari hiyo kupata hasara na kulazimika kukodi Tug ya
kupakuwa mizigo kutoka nangani kwenye meli hadi katika pwani ya
bandari hiyo.
“Mheshimiwa mkuu wa mkoa japo agizo hilo linafaida kwa serikali lakini
tunamuomba Mheshimiwa Rais angalie upya agizo hilo kwani kuna baadhi
ya taasisi zinazojiendesha kibiashara zinaathirika na utendaji wake wa
kila siku kushuka”alibainisha Kaimu Meneja huyo.
Aliiomba serikali kuangalia namna bora ya kutenganisha taasisi hizo
katika utoaji wa vibali kwani kwa hili limesababisha kushindwa
kupelekaTug meli ya kukokotea vyombo vya majini yao kwa ajili ya
ukarabati nchini Kenya.
“Tagi tuliyonayo katika bandari ya Tanga ni mmoja pekee na manahoza
waliisimamisha kufanyakazi toka mwezi Novemba mwaka jana hivyo
tumelazimika kukodi Tug kutoka mjini Mombasa ili kurahisisha utoaji wa
mizigo”alisema Arika.
Ambapo aliongeza kuwa hali hiyo situ inakwamisha utendaji kazi bali
inachangia hasara kwa Mamlaka kwani hulazimika kutumia gharama kubwa
kwaajili ya uwendeshaji kifaa cha kukodisha.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza alisema kuwa uwamuzi
wa Rais ni kwa ajili ya kuhakikisha maendeleo ya nchi yanapatikana kwa
haraka na kwa kutumia raslimali kwa uwangalifu.
Alisema kuwa sambamba na hilo ilikuweza kuongeza ufanisi katika
bandari ameahidi kuunda tume itakayokuwa ikishughulika na kutatua kero
mbalimbali zinazoikabili bandari hiyo kwa lengo la kuongeza ufanisi .
MWISHO
Post a Comment