Baadhi ya wananchi na viongozi wa kijiji cha Ngunichile, wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi. Wameiomba serikali kuharakisha na kukamilisha mchakato wa uvunaji wa msitu wa kijiji hicho.
Wananchi na viongozi hao waliyasema hayo mbele ya timu ya waandishi wa habari na maofisa wa Mtandao wa jamii wa usimamizi wa misitu (MJUMITA) waliokwenda kijijini hapo juzi ili kuona mafanikio na changamoto za uhifadhi misitu.
Waliiambia Lindiyetu.com urasimu ambao hawaujui unatokana nanini, umesababisha uvunaji wa mazao ya misitu kwenye msitu waliohufadhi uchelewe kuanza.
Bakari Lilombo aliyejitambulisha ni mwanajamii, alisema kutoanza uvunaji wakati miti imefikia umri wa kuvunwa kunasababisha baadhi ya wananchi kukatatamaa kutokana na kutoona manufaa ya msitu huo."Uvunaji ungeanza ungeingiza mapato ambayo yangetumika kununua zana za kilimo na kujenga visima vya vya maji, lakini kwa hali hii tunakata tamaa,"alisema Bakari.
Mzee Hamis Malombe mwanajamii, alisema matarajio ya wananchi nikunufaika na mapato ya mazao ya msitu huo wenye hekta 1800, kupitia huduma za jamii. Hata hivyo wananchi wanakata tamaa na matarajio yao yameanza kutoweka.
Bi Maua Ntila, ambae ni mjumbe waserikali ya kijiji hicho, alisema mapato ambayo yangetokanana mauzo mazao ya msitu huo yangeweza kutumika kuchimba visima na kuboresha zahanati. Jambo ambalo lingekuwa ni ukombozi kwa akinamama wakazi wa kijiji hicho.
Hatahivyo hadi sasa hawajaanza uvunaji, ingawa walitaraji uvunaji ungekuwa umeanza tangu mwaka jana. Kwa upande wake, ofisa mtendaji wa kijiji hicho, Selemani Soya, alisema hatua za awali za maandalizi ya uvunaji zilishafanyika.
Ofisi ya mkurugenzi wa wilaya ya Nachingwea iliwahaidi wangeanza uvunaji mwaka jana mwezi novemba, hata hivyo hadi sasa hawajaanza kuvuna."Tunapata shida ya kupambana na wavunaji haramu,maana maeneo mengi hayana miti" kwahiyo eneo lenye miti ni msitu huu, kama tungeanza uvunaji naamini wangeogopa na tungekuwa na nafuu sana,"alisema Selemani.
Akijibu malalamiko hayo kwaniaba ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Nachingwea. Ofisa misitu wa halmasiauri hiyo, Paiton Kamnana, alisema uvanaji umechelewa kuanza kwasababu kutokamilika baadhi ya taratibu, nyaraka na nyundo.
Hata hivyo maandalizi yote yamekamilika, kwahiyo muda si mrefu uvunaji utaanza.
"Nyaraka zilishafuata wizarani,nyundo imeshapatikana pia.Ilikuwa jambo lisilowezekana kuanza uvunaji kabla ya kuwapa plan(mpango)".
Utunzaji wa msitu huo nimatokeo ya elimu iliyotolewa na mashirika yasiyo kiserikali ikiwamo Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania(MJUMITA) kupitia mradi wa kampeni ya mama misitu kwa kushirikiana na serikali.
Post a Comment