Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mexico imeanza rasmi utaratibu wa mahakama wa kutaka mlanguzi wa dawa za kulevya Joaquin "El Chapo" Guzman apelekwe Marekani kujibu mashtaka.
Serikali imesema maafisa wa polisi wa Interpol wamemkabidhi stakabadhi za mahakama katika gereza la Altiplano, karibu na jiji la Mexico City.
Guzman, 58, alitoroka gerezaji mwezi Julai mwaka jana lakini akakamatwa Ijumaa.
Mexico pia inatafakari uwezekano wa kumchunguza mwigizaji wa Hollywood Sean Penn, aliyemhoji Guzman baada yake kutoroka jela.
Maafisa wa Mexico, ambao hawakutaka kutajwa, wamesema mikutano ya kisiri kati ya Penn na Guzman ilisaidia kukamatwa kwake.
Kwenye makala iliyochapishwa kwenye jarida la Rolling Stone, kutokana na mahojiano hayo yaliyodumu masaa saba, Penn na Guzman wanajadili mambo mengi yakiwemo ulanguzi wa dawa za kulevya.
Mexico ilianza utaraibu wa kutaka Guzman asafirishwe hadi Marekani mwaka 2014 kufuatia ombi kutoka kwa Marekani.
Kupitia taarifa, afisi ya mwanasheria wa Mexico imesema maajenti wa Interpol nchini Mexico walifika kwa Guzman mahakani kumkabidhi vibali viwili vya kukamatwa kwake.
Marekani inataka El Chapo ajibu mashtaka ya kuingiza kiasi kikubwa cha mihadarati nchini Marekani.
Guzman, aliyetajwa na Tume ya Kukabiliana na Jinai ya Chicago ya 2013 kama Adui Nambari Moja wa Umma, amefunguliwa mashtaka katika mahakama saba nchini Marekani.BBC

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top