Kaimu Mkurugenzi jiji la Mbeya Dkt Samuel Lazaro akizungumzia zoezi hilo mbele ya wandishi wa habari
Na Mwandishi wetu,Mbeya
Halmashauri ya jiji la
Mbeya imeanza kuwachukulia hatua kali wale waliokaidi agizo la upandaji wa
mazao yenye urefu wa mita moja pembezoni mwa makazi yao ,hususani mahindi na
mtama.
Hatua hiyo ni pamoja na kufyeka mazao hayo pamoja na kulipa
faini ya shilingi elfu hamsini kila atakae kutwa katika eneo lake .
Akizungumza na Ofisni kwakwe Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya
jiji la Mbeya Dkt Samuel Lazaro amesema halmashauri hiyo ilikwisha toa wito kwa
wananchi kuacha kupanda mazao pembezoni makazi yao laikini baadhi yao walikaidi
agizo hilo.
Amesema kutokana wananchi kugaidi agizo hilo wao kama
halmashauri wameamua kufuata sheria kwa kuanza zoezi la kufeya mazao hayo
sanjali na kuwatoza faini ya shilingi elfu hamsini .
Dkt Lazaro amezitaja baadhi ya kata zilizo athirika na zoezi
hilo ni pamoja na Sisimba,Maendeleo ,Majengo,Ghana,Sinde,Isanga na Mbalizi
road.
Nyingine ni Ruanda ,Forest Mpya ,Ilomba,Manga ,Ilyela
,Mwakibete ispokuwa mitaa ya Ilembo na Iyela
Amesema kupanda Mahindi au mtama karibu na makazi ya watu ni
kuhatarisha usalama kwani asilimia kubwa ya vitendo vya kihalifu vimekuwa
vikihusisha na uwepo wa hali hiyo hivyo amewataka wananchi kutoa ushirikiano
ili kufanikisha zoezi hilo.
Mwisho.
|
Post a Comment