Mwanafunzi wa chuo kikuu raia wa
Iraq katika jimbo la California nchini Marekani anasema kuwa alitolewa
kutoka ndege ya shirika la ndege la Southwest baada ya kufanya
mazungumzo kwa lugha ya kiarabu.
Shirika hilo la Southwest lilisema kuwa Khairuldeen Makhzoomi aliondolewa tarehe 9 mwezi Aprili baada ya ndege hiyo kupaa.Bwana Makhzoomi anasema alikuwa akizungumza na mjomba wake kwa njia ya simu kuhusu hotuba ya katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon.
Bwana Nmakhzoomi anasema kuwa mwanamke mmoja kwenye ndege hiyo alimkodolea macho wakati alitumia jina "inshallah" akimaanisha Mungu akipenda.
Baada ya kutumia jina hili mfanyikaziawa shirika la Southwest alimsindikiza nje ya ndege.
Bwana Makhzoomi ambaye aliingia nchini Marekani kama mkimbizi kutoka Iraq na sasa ni mwanafunzi wa chuo cha Carlifonia cha Berkeley , aliambiwa kuwa hawezi kuingia kwenye ndege hiyo.
Post a Comment