Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF), Issa Hayatou amemtumia salamu za pongezi Ravia Idarous Faina kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) mwishoni mwa juma lililomalizika.
Katika salamu zake, Hayatou amesema kwa niaba ya CAF, Kamati ya Utendaji na yeye binafsi wanampongeza kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA).
CAF wanaimani na uzoefu wa Ravia katika uongozi, kuwa ataendeleza uongozi bora kwa faida ya maendeleo ya soka visiwani Zanzibar.
Aidha Hayatou amewatumia pia salamu za pongezi, Mzee Zam Ali na Ali Mohamed kwa kuchgauliwa kuwa makamu wapya wa Rais wa ZFA.
Hayatou amewatakia mafanikio mema katika nafasi mpya hizo walizochaguliwa na kuahidi CAF itaendelea kuwapa ushirikiano wa maendeleo ya mpira wa miguu visiwani Zanzibar.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top