Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Galawa akizungumza katika mkutano huo. |
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na
Michezo, Nape Nnauye amesema uamuzi wa serikali kuzuia matangazo TBC kutokurusha mojakwamoja(live) matangazo ya Bunge ilikuwa
na lengo la kulinusuru shirika hilo lisife
kwani lilikuwa likitumia fedha nyingi kwa ajili ya matangazo hayo .
Amesema uamuzi huo ni mkakati wa
kuliwezesha shirika hilo kuweza kujiendesha kwani awali lilikuwa likitumia
fedha nyingi kwa urushaji wa matangazo ya bunge bila ya malipo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii
na Michezo, Nape Nnauye, amesema hayo jijini Mbeya, wakati akizungumza na wadau
wa habari,michezo, utamaduni na watendaji wa serikali Mkoa wa Mbeya na Songwe,
Amesema Shirika la utangazaji TBC,
lilikuwa linaagizwa kurusha matangazo ya bunge bila ya malipo ambapo kwa mwaka
shirika lilikuwa likitumia Bilioni 4 kwa mapato yake ya ndani na kulifanya
kushindwa kukarabati mitambo pamoja na mslahi ya watumishi hivyo hivyo uamuzi
huo ulikuwa sahihi licha ya wengi kuonesha kutolidhishwa no.
Amesisitiza kuwa suala hilo litaleta
heshima ya Bunge kwani ilifika wakati, baadhi ya wabunge walikuwa wakitoa lugha
za maudhi pamoja na kucheza sarakasi mambo ambayo yalikuwa yakivunja heshima ya
bunge.
Amesema kutokana na hatua hiyo Bunge lenyewe ndio limechukua dhamana ya
kuanzisha Studio yake hivyo kutoa fursa kwa Televisheni nyingine kurusha
matangazo ya moja kwa moja lakini kulingana na vigezo na masharti
yatakayohalalishwa na mamlaka hiyo husika.
Akizungumzia
sheria ya baraza la michezo ambayo imekuwa ikilitaja suala la michezo ni hiari
na si uchumi, Nape amesema kwa sasa serikali ipo katika mchakato wa
kuirasimisha sheria hiyo ili iendane na sera ya michezo ambayo imeweka wazi
kwamba michezo kuwa shughuli rasmi ya kiuchumi.
ambapo katika kikao hicho wajumbe
walipata nafasi ya kuwasilisha kero na changamoto mbalimbali wanazokumbana
nazo.
Aidha, akijibu risala iliyotolewa na
Chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Mbeya, ambayo ilimuomba kiongozi huyo
kuhakikisha anausimamia mswada huo wa habari katika kulinda maslahi ya
wafanyakazi,Nape, aliwataka waandishi wa habari kutambua kuwa maslahi yao
wanayoyapigania kutoka kwa waajiri wao, yanajibiwa kwenye mswaada wa sheria ya
huduma wa vyombo vya habari.
Alisema, wakati ule ulikuwa ni
mwishoni mwa Bunge lililopita hivyo kwa sheria na kanuni za Bunge mswaada huo
unatakiwa ukasomwe tena kwa mara ya kwanza, kwa hiyo umefikia pahala pazuri, na
kuhakikisha kwamba maslahi ya waandishi wa habari mule ndani yamelindwa.
Pia, Waziri huyo, aliongeza kuwa
serikali inaangalia utaratibu wa kuvifuta baadhi ya vyuo vinavyotoa elimu
ya habari ambavyo havina sifa, kwani vimekuwa vikitoa waandishi wa habari
amaboa hawana sifa na kazi yao imekuwa ni kuupotosha umma.
Mwisho.
Imeandaliwa na Mtandao wa Kijamii wa www.Jamiimoja.blogspot.com/0759406070
Mbeya.
Post a Comment