Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akizungumza wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na  benki ya NMB kwa wananchi mkoa wa Mbeya Royal Tughimbe jijini Mbeya June 30 mwaka huu.
Wananchi wa jiji la Mbeya  wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa mbeya Amos Makalla wakati wa   hafla ya futari iliyoandaliwa na benki ya NMB kwa wananchi mkoa wa Mbeya



Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla wa pili kushoto akipata chakula  na viongozi wa dini ya Kislam na wageni waalikwa  katika  hafla ya futari iliyoandaliwa na  benki ya NMB kwa wananchi mkoa wa Mbeya.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akifurahi jambo wakati akipata chakula katika hafla ya futari iliyoandaliwa na benki na benki ya NMB kwa wananchi mkoa wa Mbeya

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ameipongeza benki ya Nmb kwa huduma Bora kwa wateja nchini na uchangiaji wa huduma za jamii ikiwemo elimu na Afya hapa nchini
Hayo ameyasema leo wakati hafla ya futari iliyoandaliwa na benki na benki ya NMB kwa wananchi mkoa wa Mbeya
Amesema benki ya Nmb imekuwa mstari wa Mbele katika uchangiaji wa madawati na sekta ya afya kwa mujibu wa taarifa benki imetumia shilingi bilioni 1.5 katika mambo ya kijamii
Amewashukuru Nmb kwa uamuzi wa kuwafuturisha wananchi Mkoa Mbeya na amewatakia mafanikio ktk shughuli za kibiashara na amewahamasisha wananchi kuitumia benki ya NMb
Aidha amewataka viongozi wa dini zote kushirikiana ili kudumisha amani na mshikamano

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top