Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akitoa Nasaha maalum mara baada ya kumaliza kufuturu na watoto Yatima
kwenye viwanja vya Karimjee iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate Princess
inayoandaa kipindi television cha Mboni Show.
Mkuu wa Wilaya ya kinondoni Mhe. Ally Hapi (kushoto) akiwa kwenye dua pamoja na wageni waalikwa wengine.
Watoto
Yatima wakiswali wakati wa tafrija ya kufuturisha watoto Yatima
iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa kipindi cha
televisheni cha Mboni Show ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na kufanyika
kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kushoto) akisalimiana na Mkuu mpya wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema (kulia) mwingine pichani ni Mkurugenzi wa kampuni ya Chocolate Princess inayotengeneza kipindi cha television cha Mboni Show Bi. Mboni Masimba wakati wa tafrija ya kufuturisha watoto yatima iliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee.
Mkurugenzi wa kampuni ya Chocolate Princess kinachoandaa kipindi cha The Mboni Show akizungumza wakati wa kufuturisha watoto yatima .
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Mhe. Paul Makonda akizungumza kwenye tafrija ya kufuturisha Watoto Yatima
iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa na kipindi cha
television Mboni Show ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Watoto wakipewa juisi wakati wa Tafrij ya Futari.
Naibu Mufti Mkuu Sheikh Hamid Jongo akizungumza kwenye tafrija hiyo.
................................................
................................................
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali
inaendelea kuvisimamia kwa ukaribu vituo vyote vya kulelea watoto yatima nchini
na vituo ambavyo vitabainika kuwa vinanufaisha wamiliki na vinaendeshwa bila ubora vitafungiwa mara moja.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam katika hafla
ya futari iliyoandaliwa na Kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa kipindi cha
Mboni Show hafla iliyojumuisha watoto yatima
283 kutoka Vituo vitano vya Mkoa wa Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais amesema kuwa azma ya serikali ni kuona vituo vyote vya kulelea watoto
yatima kote nchini vinatoa huduma bora na inayokidhi mahitaji ya watoto hao na
sio vinginevyo.
Kuhusu
malezi ya Watoto yatima, Makamu wa Rais ametoa wito kwa jamii iendelee kusaidia
watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi kwa kuwapatia elimu
bora,upendo na si kuiachia serikali mzigo huo au mashirika yasiyo ya kiserikali.
Aidha,
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameiomba jamii kuweka mipango mizuri ya
kukabiliana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto yatima kwa kuwa
nao wana haki ya kuishi vizuri kama watoto wengine.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Post a Comment