Mkuuwa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akiwaapisha wakuu wa wilaya wapya(wateule) katika ukumbi wa mkapa jijini Mbeya Julai4 2016. |
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amewataka wakuu wapya wa wilaya kuifanya siku ya alhamis ya kila wiki kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi wa haraka na muhutasari huo umfikie mezani kila Jtatu ya kila wiki
Amesema baadhi ya wananchi wanachukia serikali kutokana na kutopatiwa majibu ya changamoto zao na urasimu baadhi ya viongozi na watendaji hivyo ni vema siku hiyo moja katika wiki ikawa siku ya wazi kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi tu kama ambavyo yeye Mkuu wa mkoa alivyotenga siku ya Alhamis ya mwanzo wa mwezi na Alhamis ya mwisho wa mwezi ni kwa ajili ya kusikiliza Kero za wananchi
Amewataka kupitia kamati za ulinzi na usalama wadumishe amani na utulivu na kudhibiti vitendo vya uhalifu na ujambazi wa kutumia silaha
Aidha amewaagiza kufuatilia na kuhamasisha shughuli za maendeleo na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha kwa miradi inayotekelezwa katika halmashauri zao
Mkuu wa Wilaya Amos Makalla akizungumza katika hafla hiyo ya kuwaapisha wakuu wapya wa wilaya katika ukumbi wa Mkapajini mbeya Julai 4 mwaka huu. |
Picha ya pamoja |
Post a Comment