Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akizungumza katika mkutano na baraza la Madiwani Halmashauri ya jiji la Mbeya .
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ametoa siku saba kwa Mkuu wa wilaya na mkurugenzi wa Jiji la Mbeya kuyaondoa magari yote ya mizigo yanayapark pembezoni mwa Barabara mwa Barabara kuu kinyume na utaratibu wakati kuna vibao vinaeleza ni marufuku magari ya mizigo kupark maeneo hayo." Siwezi kuendelea kuona magari yamejazana hapa kuna vibao vinakataza lakini watu hawatii makatatizo hayo madiwani mpo, viongozi mpo, takataka zinazagaa watendaji mpo, viongozi tupo kuanzia leo usafi wa jiji letu ni sehemu ya kipaumbele na kwa kuanza magari yote ya mizigo ndani ya wiki moja yaondoke yapelekwe eneo lililotengwa "
Hayo ameyasema leo katika kikao cha pamoja na madiwani na watendaji wa jiji la Mbeya wakati wa kujadili taarifa ya mkaguzi na mdhibiti wa serikali( CAG)
Kuhusu ukusanyaji wa mapato amewataka watendaji na madiwani kudhibiti mapato kwa kuhakikisha mapato yote yanakusanywa kwa njia ya elektroniki
Aidha amewataka madiwani kukagua miradi ili miradi hiyo iliyojengwa ieandane na thamani ya Fedha
Madiwani halmashauri ya jiji la Mbeya wakiwa makini kumsikiliza mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla (hayupo pichani) katika ukumbi wa halmashauri ya jiji la Mbeya.

Amos Makalla Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ,mwenye suti akisalimiana na Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi na viongozi wengine.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top