Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony J. Mtaka akizungumza na Viongozi na Maafisa Kilimo wa mkoa huo(hawapo pichani) katika kikao kilichofanyika mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mwelekeo wa sekta ya kilimo kama kipaumbele cha pili Mkoani Simiyu kwa mwaka huu, (kushoto) Kaimu Katibu Tawala Mkoa, Bw. Donatus A. Weginah
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony J. Mtaka (katikati) akizungumza na Viongozi na Maafisa Kilimo wa mkoa huo (hawapo pichani) katika kikao kilichofanyika mjini Bariadi kikiwa na lengo la kujadili mwelekeo wa sekta ya kilimo kama kipaumbele cha pili Mkoani Simiyu kwa mwaka huu, (kushoto) Kaimu Katibu Tawala Mkoa, Bw. Donatus A. Weginah na (kulia) Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga
Viongozi na Maafisa kilimo wa Mkoa wa Simiyu, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Anthony J. Mtaka (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mwelekeo wa sekta ya kilimo kama kipaumbele cha pili Mkoani Simiyu kwa mwaka huu.


         Na Stella Kalinga (Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu)

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony J. Mtaka amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani humo kutenga bajeti kwa ajili ya kuwawezesha Maafisa kilimo wa Vijiji,Kata na Wilaya kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Mtaka ametoa agizo hilo wakati alipokuwa akizungumza na Viongozi na Maafisa Kilimo katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ambacho kilihudhuriwa na Wakuu wa wilaya,Wenyeviti wa Halmashauri,Wakurugenzi na Makatibu Tawala Wilaya kutoka  katika wilaya zote tano za mkoa huo.

Mtaka amesema Maafisa Kilimo wanapaswa kuwezeshwa kwa kupewa vyombo vya usafiri kama pikipiki na magari pamoja na mafuta, ili waweze kuwafikia wakulima katika maeneo yao kwa ajili ya kuwapa ushauri wa kitaalam kila wanapowahitaji katika kuendeleza kilimo bora na chenye tija.

“Mwaka huu kilimo kwa mkoa wetu ni  kipaumbele cha pili na Halmashauri za Mkoa huu zinategemea kilimo kwa takribani asilimia 90 ya mapato yake ya ndani, ipo haja  kuwawezesha maafisa kilimo kwa kuwa wana mchango kubwa katika mapato ya Halmashauri. Ningependa kuona mwaka 2016/2017 hadhi ya Maafisa Kilimo inapanda, Wakurugenzi muwathamini hawa wataalam ndiyo wanaowasaidia kupata hayo mapato katika pamba, choroko, dengu, mpunga na mazao mengine”, alisema Mtaka.


Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top