Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mwanamitindo mwenye ndevu za urefu wa inchi sita ametambuliwa na Guinness World Record kuwa mwanamke wa umri mdogo zaidi duniani kuwa ndevu zilizokomaa kabisa.
Harnaam Kaur, 24, ambaye ni mwanamke mtetezi wa kutambuliwa na kukubalika kwa hali ya mwili wa mwanadamu ulivyo bila ubaguzi anatoka Slough, Berkshire nchini Uingereza.
Amesema ni heshima kubwa kwake kutambuliwa.
Ameeleza ndevu hizo ndefu kama sehemu ya juhudi zake za kukabiliana na watu wengi waliomkejeli kutokana na muonekano wake.
Wengine waliotambuliwa kwenye rekodi za karibuni zaidi ni paka mrefu zaidi anayefugwa kama mnyama kipenzi pamoja na Ilama anayeruka juu zaidi.

Bi Kaur ana tatizo la homoni lifahamikalo kwa Kiingereza kama polycystic ovary syndrome, ambalo humfanya mwanamke kuwa na nywele zaidi kuliko kawaida usoni.
Machi 2016 Harnaam Kaur alikuwa mwanamke wa kwanza kushiriki maonyesho ya mitindo ya London Fashion Week akiwa na ndevu.BBC

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top