Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti John Wanyancha,akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza kuhusu mpango wa kampuni hiyo kuwawezesha wakulima wa hapa nchi wanaozalisha malighafi zinazotumika kiwandani kwao,ambapo wakulima wapatao 100 wamenufaika katika mkutano uliofanyika mapema leo katika kiwanda cha SBL Mwanza.





Waandihsi wa habari wakifuatilia kwa makin maelezo toka kwa Mkurungezi wa mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti John Wanyancha mapema leo katika kiwanda cha SBL Mwanza.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti John Wanyancha,akiongoza waandishi wa habari kutembelea baadhi ya maeneo ya kiwanda cha SBL Mwanza.


</ tr>
Meneja wa upishi wa bia wa Kiwanda cha Serengeti Rolinda Samson(Brewing Manager) akitoa ufafanuzi wa jambo jinsi utengenezaji wa bia unavyofanyika kwa  waandishi wa habari jijini Mwanza mapema leo.





Mwanza, Septemba 07, 2016 - Hamasa inayotokana na mradi wa kilimo biashara wa kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kwa kuwawezesha wakulima wa mahindi, mtama  na shayiri katika maeneo mbalimbali nchini  imewezesha kampuni hiyo ya bia kuongeza kiwango cha malighafi   inayotumika  kutoka ndani ya nchi kufikia  tano 10,000 sawa na asilimia 60  ya malighafi yote inayotumia   kuzalisha bia kwa mwaka.


Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari  uliofanyika katika kiwanda cha SBL  Mwanza leo,  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, John Wanyancha  alisema& nbsp; aina   sita za bia zinazozalishwa na kampuni hiyo zina asilimia 100  ya malighafi inayoizalishwa   ndani  ikiwa ni matokeo ya mradi wa kilimo biashara  ambao ulianza  miaka mitatu iliyopita.


Aina hizo za bia ni pamoja na Pilsner, Kibo Gold, Kick, Uhuru na Senator Lager.  Kwa mujibu wa Wanyancha  bia mbili za Pilsner na Kibo Gold  zimeshinda tuzo  za kimataifa mwaka huu ikiwa ni kielelezo cha ubora wa hali ya juu wa bidhaa hizo..


Kupitia programu hiyo kampuni ya Bia ya Serengeti  inatoa mbegu zilizo na ubora  kwa wakulima bure, kuwaunganisha na taasisi za kifedha  ili kupata mitaji   inayohitajika  kwa ajili ya kilimo  cha mashamba makubwa  hali kadhalika   kuwaunganisha na wasambazi wa mbolea na dhana nyninginezo za kilimo. Kwa upande wake SBL imekuwa ikinunua  mazao yote  kutoka kwa wakulima hawa na hivyo kuwawezesha kulipa mikopo ya mitaji pamoja na kuboresha hali zao za kiuchumi.


“Hadi sasa  mradi huu umeshawanufaisha   wakulima zaidi ya 100 kutoka mikoa kadhaa ikiwemo Arusha, Manyara, Mbeya, Kilimanjaro, Singida, Morogoro, Shinyanga na  Dododoma ambao kwa pamoja wanalima takribani ekari 20,000,”  alisema mkurugenzi huyo.


Wanyancha alisema  kwamba kampuni hiyo  imepanga kuendelea kupanua programu hiyo  ili kuwafikia wakulima wengi zaidi ili kufikia lengo  la kuongeza upatikanaji wa malighafi kutoka ndani hadi asilimia 80 kwa mwaka huu. Mbali na manufaa mbalimbali ya kichumi kwa wakulima, bali zitokanazo na malighafi zinazozalishwa nchini  ni za bei nafuu ikilinganishwa na zile zinazotengeneza na malighafi kutoka nje ya nchi.


Mwisho</ div>

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top