Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
(kushoto) akiongoza na mwenyeji wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida mara baada ya
kuwasili kwenye ofisi za ESRF kufungua warsha ya nafasi ya wazee katika
kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF
kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International.
Mkurugenzi
Mkazi Shirika la kimataifa la kusaidia wazee (Help Age International),
Amleset Tewodros (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu (wa
pili kulia) ofisini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa
Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (katikati). Wengine kushoto ni
Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini na Kuinua Uchumi kutoka Wizara ya
Fedha na Mipango, Anna Mwasha na Mkurugenzi Mkazi Msaidizi wa Shirika la
kimataifa la kusaidia wazee (Help Age International), Smart Daniel (wa
pili kushoto).
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi
Kida akitoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi na washiriki wa warsha ya
nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs)
iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age
International iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar
es Salaam.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
akifungua warsha kuhusu nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya
maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na
Shirika la Help Age International na kufanyika katika ukumbi wa mikutano
wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi
wa Jukwaa la Wazee Tanzania, Samson Msemembo (85) akizungumzia
changamoto wanazokutana nazo wazee katika vituo vya huduma za afya kwa
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy
Mwalimu (katikati), Kaimu Kamishna Ustawi wa Jamii Bw.Rabikira Mushi
kutoka Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
(kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi
na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida waliopo meza kuu.
Mtafiti
Mkuu Mshiriki kutoka Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF) na
Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Oswald Mashindano akizungumzia
nafasi ya wazee katika sera ya kitaifa kwenye warsha kuhusu nafasi ya
wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs)
iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age
International iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar
es Salaam.
Mkurugenzi
Mkazi Shirika la kimataifa la kusaidia wazee (Help Age International),
Amleset Tewodros akishiriki kutoa maoni kwenye warsha kuhusu nafasi ya
wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs)
iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age
International na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar
es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi
Kida akifafanua jambo kwenye warsha ya nafasi ya wazee katika kutekeleza
malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa
kushirikiana na Shirika la Help Age International. Kushoto ni Mkurugenzi
Mkazi Shirika la kimataifa la kusaidia wazee (Help Age International),
Amleset Tewodros.
Mshauri
wa Masuala ya Ushirikiano wa Kanda ya Afrika Mashariki, Kati na
Magharibi wa Shirika la Help Age International, Roseline Kihumba
akizungumzia hali ya uzee na wazee duniani na ushirikishwaji wa wazee
katika maendeleo endelevu kwenye warsha ya nafasi ya wazee katika
kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF
kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International.
Mkurugenzi
wa Kupunguza Umaskini na Kuinua Uchumi kutoka Wizara ya Fedha na
Mipango, Anna Mwasha akichangia mada kwenye warsha ya nafasi ya wazee
katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na
ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Uchambuzi wa Sera na Utafiti wa Wizara ya Fedha na
Mipango, Mudith Cheyo akifafanua jambo kwa washiriki wa warsha kuhusu
nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs)
iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age
International.
Mkurugenzi
wa Mtandao wa Watu Waishio na Virusi vya Ukimwi Tanzania (SHDEPHA),
Joseph Katto akizungumzia changamoto zinazowakabili wazee wanaoishi na
VVU katika kupata huduma mbalimbali nchini kwenye warsha kuhusu nafasi
ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs)
iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age
International na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar
es Salaam.
Sehemu
ya washiriki waliohudhuria warsha kuhusu nafasi ya wazee katika
kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF
kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International na kufanyika
katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa mikutano wa ESRF
wakati wa warsha kuhusu nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya
maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na
Shirika la Help Age International
Picha ya pamoja
Na Mwandishi wetu
SERIKALI
ya Tanzania imeshauriwa kuhakikisha kwamba kunakuwapo na ushirikishaji
wa wazi wa wazee katika sera na mipango ya maendeleo.
Aidha imetakiwa kutoa nafasi kwa wazee katika utekelezaji wa miradi yake ya maendeleo, jamii na mazingira.
Kauli
hizo zimetolewa na washiriki wa warsha ya nafasi ya wazee katika
kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu ,SDGs ambayo imeingizwa katika
mipango ya maendeleo ya taifa.
Wakiongozwa
na mada mbalimbali zilizotolewa na wataalamu mbalimbali kama Dk Oswald
Mashindano, Danford Sango, Ahmed Makbel, Dk. Ntuli Kapologwe washiriki
walisema kwamba ingawa Tanzania ina sera nzuri kuhusu wazee utekelezaji
wake umekuwa wa kusuasua kutokana na kukosekana kwa utashi.
Aidha
walisema kwamba kukosekana kwa sheria ya wazee kunawafanya wazee hao
kunyanyasika hasa katika masulaa ya kiuchumi na kiafya.
Joseph
Kato (62) ambaye alisema kwamba amekuwa akiishi na UKIMWI tangu ujana
wake hadi sasa ameingia rasmi katika rika la wazee, anasema kwamba sera
za nchi hasa za afya haiztoa umuhimu kwa magonjwa kama Ukimwi.
Aidha
alisema kwamba wazee wakiwa na afya zao wamekuwa wakipuuzwa katika
suala la uchumi kwani ukiwa unaishi na Virusi vya Ukimwi ukienda benki
hupewi mikopo na pia ukiwa mzee hupewi mikopo.
Alisema
kama sera ni kuhakikisha hakuna anayeachwa katika safari za utekelezaji
wa maendeleo endelevu ipo haja kwa serikali kuhakikisha kwamba wazee
hawanyanyaswi na wanasaidiwa kuwezeshwa kiuchumi.
Mshiriki
mwingine aliyejitambulisha kama Mama Koku alisema kwamba ngazi za chini
za utekelezaji zimekuwa hazitoi kipaumbele kwa wazee japo serikali kuu
katika mipango yake imeonesha nini kinachotakiwa kufanywa na kila mmoja
katika nafasi ya kuhudumia wazee.
Alisema
upo mkakati wa mwaka 2007 hadi 2025 ambao umeonesha utekelezaji wa
huduma kwa makundi tete lakini wakurugenzi wa halmashauri hawaweki wazee
kama kipaumbele chao wakisingizia serikali kuu.
Hata
hivyo amesema wakati umefika kwa serikali kufuatilia mkakati huo kwa
lengo la kuwabana wahusika ili kipaumbele kwa wazee kiwepo.
Amesema
maofisa mipango wengi wanakwepa kuweka kipaumbele kwa dai kuwa fedha
wanazoletewa ukomo wake hauruhusu kuwaingiza wazee huku wengine
wakidanganya kwamba serikali kuu ndio imeondoa msaada kwa wazee.
Naye
Ishaka Msigwa kutoka Ruvuma alisema kwamba tatizo kubwa la kuhudumia
wazee sio sera kwani ipo ila dhamira ndio haipo. Alisema wazee
wanataabika sana katika suala la uchumi na kwamba ipo haja sheria ya
wazee ikatungwa ili kuwasaidia kuondokana na adha ya kukataliwa wakati
wa kutafuta mikopo ya kuwainua kiuchumi.
Alisema asilimia 50 ya mayatima wanakaa na wazee vijijini na kitendo cha kuwanyima ushiriki wa uwezeshaji unawatesa.
Pamoja
na malalamiko hayo ya wazee ambayo yalijikita katika kuwa na kipato
cha uhakika na suala la upatikanaji wa matibabu, serikali ilisema
imekamilisha utaratibu wa utoaji wa pensheni kwa wazee Tanzania bara na
kinachosubiriwa kwa sasa ni utekelezaji wake.
Waziri
wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
akifungua warsha hiyo kuhusu nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo
ya maendeleo endelevu (SDGs) alisema hata hivyo serikali itaanza kutoa
posho hizo kwa wazee wa miaka 70 kwenda juu na badae watashuka hadi
katika umri unaokubalika.
Alisema wamejifunza kutoka Zanzibar na wanaona hapo ni eneo jema la kuanzia.
Aidha alisema kwamba bado anaendelea na juhudi zake za kutaka sheria ya wazee itungwe kwa kuwa ipo sera inayohusu wazee.
Kwa hesabu za karibuni Tanzania inawezee zaidi ya milioni 2.
Pamoja
na kuzungumzia suala la malipo ya pensheni ambapo alisema suala hilo
kwa sasa lipo Hazina, waziri huyo alirejea msisitizo wake wa kutaka
wazee watibiwe bila malipo.
Alisema
serikali ya awamu ya tano ni serikali ya utekelezaji na kwamba suala la
tiba bure kwa wazee ni suala la sera na wala si utashi.
Akizungumza
kwa kina masuala yanayogusa wazee kama yalivyotolewa kwa sauti na mzee
Samson Msemembo (85), Waziri Ummy alisema kwamba serikali inatambua
changamoto zinazowakumba wazee na itazifanyia kazi kuhakikisha kwamba
zinapatiwa majibu.
Mzee
Msemembo kutoka Jukwaa la wazee Tanzania, alisema kwamba wazee wamekuwa
wakinyanyasika katika sekta ya afya na uchumi wakibaguliwa na kunyimwa
fursa za kuishi kwa furaha.
Akizungumza
kuhusu kero zilizoelezwa katika warsha hiyo iliyoendeshwa kwa pamoja
katika Taasisi za Tafiti za Kiuchumi na Kijamii nchini (ESRF) na taasisi
ya kimataifa ya kusaidia wazee Help Age, Waziri Ummy alisema serikali
inataka wazee wawe na kipato cha uhakika na kupewa matibabu.
Amesema
hakubaliani na suala la wazee kukosa matibabu na kutaka wakurugenzi
wote wa halmashauri kuhakikisha kwamba wazee wanaingizwa katika mfumo wa
matibabu wa CHF au wanapewa kadi maalumu ya matibabu bure.
Alisema
kwamba haingii akilini kuona kwamba wazee sita katika watu 100 wanakosa
kutibiwa kwa dai la kukosekana kwa fedha wakati sera zipo zinazotaka
watibiwe bure.
Akizungumzia
tatizo la Hospitali ya Taifa Muhimbili kutotibia wazee alisema kwamba
atalishughulikia tatizo hilo kwani haliingii akilini mwake:“Watumishi,
vifaa, kila kitu ni cha serikali inakuaje wazee wasitibiwe” alihoji
Waziri Ummy .
Akizungumzia
suala la kukuza uchumi wa wazee alisema kwamba atamwandikia barua Rais
Magufuli ili aweze kutoa agizo la asilimia 2 katika mapato ya ndani ya
halmashauri kuchochea uchumi kwa wazee.
Alisema kuna asilimia 5 zimetengwa kwa vijana na wanawake pia 5 na haoni sababu zisitengwe asilimia 2 kwa ajili ya wazee.
Katika
warsha hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF Dk Tausi Kida alisema kwamba
warsha hiyo imelenga kusaidia wadau mbalimbali kutambua masuala ya wazee
katika mipango ya maendeleo kuanzia ngazi za chini ikiwa ni sehemu ya
utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu ya dunia.
Post a Comment