Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akifanya mahojiano ya kipindi maalum cha heloo Tanzania kinachorushwa
hewani na kituo cha redio Uhuru FM cha Jijini Dar es Salaam wakati wa
ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari leo Jijini humo. Kushoto ni
mtangazaji wa kipindi hicho, Sheila Simba.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan
Abbas akibadilishana mawazo na Mtangazaji wa kipindi cha heloo Tanzania
kinachorushwa hewani na kituo cha redio cha Uhuru FM, Sheila Simba
wakati wa ziara ya kutembelea vyombo vya habari leo Jijini humo leo
Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan
Abbas akibadlishana mawazo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha
Redio Uhuru FM cha Jijini Dar es Salaam, Angel Akilimali ikiwa ni sehemu
ya mwendelezo ya ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari leo Jijini
Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan
Abbas (katikati) akizungumza na wahariri na waandishi wa gazeti la Uhuru
wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari leo Jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Kaimu Mhariri Mtendaji wa Gazeti hilo, Ramdhani Mkoma
na kulia ni Afisa Habari Mwandamizi wa Idara Habari( MAELEZO), Jonas
Kamaleki.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan
Abbas akimsalimu mwandishi mwandamizi wa habari za michezo wa gazeti la
uhuru, Sophia Ashery wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya
habari leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan
Abbas akimsalimu mwandishi mwandamizi wa gazeti la uhuru, Njumai Ngota
wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari leo Jijini Dar es
Salaam.
Kaimu Mhariri Mtendaji wa gazeti
la Uhuru, Ramadhani Mkoma akimpatia maelezo kuhusu uhifadhi wa magazeti
ya zamani kwa Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas wakati wa ziara yake ya
kutembelea vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wahariri wa Gazeti la
Uhuru wakifuatilia kwa makini mkutano wa mazungumzo baina yao na
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas wakati wa ziara yake ya kutembelea
ofisi za gazeti hilo leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan
Abbas akizungumza wakati wa mkutano wake na bodi ya uhariri wa gazeti la
uhuru wakati wa ziara yake ya kutembela ofisi za gazeti hilo leo Jijini
Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Mhariri wa Picha, Yassin
Kayombo na Mhariri wa Habari Abdallah Kimweri.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan
Abbas akisalamiana na Mhariri msanifu kurasa wa gazeti la Uhuru, Jane
Mihanji mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Bodi ya Uhariri ya
gazeti hilo leo Jijini Dar es Salaam.
………………………………………..
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO.
Dar es Salaam.
SERIKALI imesema muswada wa
sheria ya huduma ya habari utatoa fursa kwa vyombo vya habari kuiomba
radhi jamii radhi kwa jamii pindi wanapoandika habari zenye upotoshaji
na hawatochukuliwa hatua za kisheria kutoka katika mamlaka zinazohusika.
Akizungumza katika mwendelezo wa
ziara yake katika vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi
wa Habari, Hassan Abbas alisema hakuna haja ya waandishi wa habari
kuuhofia muswada huo kipengele na badala yake wausome na kuelewa na
kisha watoe maoni yao ili kuuboresha zaidi.
“Sifa moja ya taaluma ya habari
ni kufuata maadili hivyo muswada umetoa fursa kwa mwanahabari kukanusha
na kueleza ulichokosea hivyo mwandishi hatashtakiwa endepo akiona
amekosea na kusahihisha ikiwemo kuomba radhi” alifafanua Mkurugenzi
Abbas.
Kwa mujibu wa Abbas alisema
kutakuwa na bodi maalumu itakayosimamia masuala ya maadili kwa waandishi
wa habari nchini na hivyo kutoa fursa kwa waandishi hao kuhojiwa na
kutoa ufafanuzi wa jambo husika.
Aidha Abbas alisema kuwa ipo
misingi ya haki ya habari iliyoanishwa katika mikataba ya kimataifa
ikiwemo kifungu cha 19 cha mkataba wa geneva wa mwaka 1966 umeeleza
kuhusu haki ya kupata habari na taarifa ingawa upo ukomo katika masuala
kadhaa ikiwemo suala la usalama wa taifa.
Aidha Abbas aliongeza kuwa
muswada huo umelenga kulinda maslahi na usalama wa wanahabari kwani
unazungumzia hali halisi ya mwandishi wa habari ukilinganisha na Sheria
ya Magazeti ya mwaka 1976 inayozungumzia haki ya chombo cha habari
pekee.
Mkurugenzi Abbas alisema kila
taaluma duniani ina bodi yake hivyo imefika wakati kwa Tanzania napo
kuwa na bodi ya wanahabari ili kuweza kuitendea haki taaluma ya habari.
Post a Comment