Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Usishangae pale utakapopokea ujumbe wa Dogo Janja akikuomba mchango wa harusi (iwapo atafanya hivyo). Ni kwasababu muimbaji huyo wa Kidebe anaweza kuwa ameshawishika kujiunga na kambi ya wavaa pete kwenye kidole cha chanda – asante kwa ushawishi alioupata kutoka kwa Tundaman.
Tunda aliuaga ukapera wiki iliyopita katika harusi iliyofanyika huko Morogoro na mchakato mzima ulimshawishi Janjaro kufikiria kufanya kitu kama hicho.
Akiongea na Clouds TV, Madee alidai kuwa Janjaro alikuwa Moro kwa takriban wiki nzima katika maandalizi ya harusi hiyo na amejifunza mengi.
Madee amesema kuna vitu vingine huenda Dogo Janja amevitamani kupitia harusi hiyo. Hata hivyo amedai kuwa hana uhakika iwapo kijana wake huyo alimaanisha kweli au aliropoka tu.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top