Katibu Mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Ndg Abdulrahman Kinana ameitumia salamu za rambirambi familia
ya Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa wa Iringa Mzee Tasili Mung’wenya Mgoda
aliyefariki dunia jana tarehe 14 Oktoba, 2016 katika Hospitali ya Wilaya ya
Mafinga.
Mzee Mgoda amewahi
kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya TANU baadae CCM na Serikalini
ambapo amekuwa Mwenyekiti wa Wilaya ya Mafinga, Katibu wa CCM ngazi ya Wilaya
na Mkuu wa Wilaya Mstaafu.
Katika Salamu hizo Ndg
Kinana amesema amepokea kwa majonzi na masikitiko makubwa kifo cha Mzee Tasili
Mgoda ambaye alikuwa ni sehemu ya hazina ya wazee wa CCM na kwamba anaungana na
familia ya marehemu, ndugu na jamaa katika kipindi hiki kigumu cha huzuni ya
kuondokewa na mpendwa wao.
WanaCCM tunamuomba
Mwenyezi Mungu aiweke peponi roho ya Marehemu Mzee Tasili Mung’wenya Mgoda. Amina
Imetolewa na:-
SELEMAN Y. MWENDA
Kny: MSEMAJI WA
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
15/10/2016
Post a Comment