Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Mshambuliaji wa Tanzania Mbwana Samatta ameshindwa kuisaidia timu yake ya KRC Genk baada ya kukutana na kipigo katika Ligi Kuu ya Ubelgiji kutoka kwa wenyeji Sporting Charleoi cha mabao 2-1.
Genk walianza kupata bao katika dakika ya 3 kupitia Nikos Karelis lakini dakika ya 11, wenyeji wakasawazisha kupitia Sotiris Ninis.
Samatta alilambwa kadi ya njano katika dakika ya 29 ya mchezo huo hata hivyo mchezaji huyu aliweza kucheza dakika zote 90.
Bao 1-1 ilikwenda hadi mapumziko na kipindi cha pili mechi ilikuwa ngumu na ilikuwa vigumu kubashiri nani atashinda.
Huku ikionekana kama mechi itaisha kwa sare, Cristophe Diandy akaumaliza mchezo zikiwa zimebaki dakika nane kwa kuifungia Sporting Charleroi bao la pili.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top