Mbunge wa Kasulu vijijini Mhe
Augustine Vuma (Kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba wakati
viongozi hao walipotembelea kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu. (Katikati
ni Bw. Peter Bulugu Kaimu Mkuu wa Kambi – Nyarugusu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akihutubia katika
Mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kagera Nkanda, Wilayani Kasulu
Sehemu ya wawakilishi wa mashirika
mbalimbali yanayotoa huduma katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu
wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mhe. January Makamba (hayupo pichani) mara baada ya
kutembelea kutembelea kambi ya Nyarugusu na kutoa maelezo katika sekta
ya mazingira
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akiwa na Mkuu wa
Wilaya ya Kasulu Kanali Martin Mkisi wakikagua uharibifu wa mazingira
katika msitu wa Makere katika Wilaya ya Kasulu
…………………………………..
Na Lulu Mussa
Kasulu
Imebainika kuwa ongezeko kubwa la
idadi ya wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu inachangia kwa kiasi kubwa
la uharibifu wa mazingira kwa kuongeza matumizi ya rasilimali za asili.
Hayo yamesemwa leo na Kaimu Mkuu
wa Kambi ya Nyarugusu Bw. Peter Bulugu wakati wa kuwasilisha taarifa ya
hali mazingira katika kambi hiyo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais anayeshughulikia masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. January
Makamba
Kaimu Mkuu wa Kambi wa Nyarugusu
Bw. Peter Bulugu amesema kuwa hali ya mazingira katika kambi si nzuri na
inakabiliwa na tatizo la uharibufu wa mazingira kwakuwa wengi wa
wakimbizi hao hutumia kuni kama nishati ya kupikia.
Hata hivyo Bw. Bulugu amebainisha
kuwa Ofisi yake imeeanda mkakati wa upandaji miti ili kunusuru maeneo
yanayozunguka, na kwakuanzia jumla ya miche 900,000 imeoteshwa katika
vitalu. Pia Kambi imedhamiria kugawa majiko banifu ambayo yatatumia
nishati kidogo na uzalishaji wa nishati kwa kutumia takataka za
mashambani unatarajiwa kuanza mwezi Novemba.
Aidha, mkakati mwingine ni ujenzi
wa nyumba za tofali mbichi na kuezeka kwa mabati badala ya miti ambapo
jumla ya nyumba 800 zimekamilika na nyumba 542 ziko katika hatua
mbalimbali za ujenzi. Alisema Bw. Bulugu
Akiwa katika Wilaya ya Kasulu
Mkoani Kigoma, Waziri Makamba ametembelea kambi ya wakimbizi ya
Nyarugusu na kupata fursa ya kuongea na wawakilishi wa mashirika
mbalimbali yanayotoa huduma katika kambi hiyo.
Waziri Makamba amesema kuwa ni
vema uongozi na mashirika yanayotoa misaada katika kambi hiyo kuandaa
mpango mzuri wa namna ya kuwapokea na kuwahifadhi wakimbizi ili ujio wao
usiathiri watanzania wanaozunguka kambi ili shughuli zao za uzalishaji
mali kila siku ziwe na tija.
Waziri Makamba aliuagiza Ungozi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi kutafuta pesa
zaidi ili mpango wa kugawa majiko banifu uwafikie wakimbizi wote. “Kaya
zilizopo hapa ni 30,000 ninyi mnataka kugawa majiko hayo kwa kaya 3000
tu, nashauri muangalie uwezekano wa kugawa kwa kaya zote” Makamba
alisisitiza.
Waziri Makamba pia ameagiza
kufanyika kwa Ukaguzi wa Mazingira (Environment Audit) ndani ya wiki
mbili kwakuwa ni takwa la kisheria. Na kuwataka na kupanda miti kwa
wingi. ” Pandeni miti ya aina mbalimbali mfao miti ya matunda, kuni na
mbao ili kunusuru mazingira yetu”.
Waziri Makamba pia alitembelea
msitu wa Makere wenye takriban ekari 75,000 ambao kwa upande wa Makere
kusini kumekuwa na uharibufu mkubwa wa mazingira na kuagiza doria za
mara kwa mara ili kudhibiti wananchi wanaofanya kilimo cha kuhamahama,
kukata na kuchoma miti pia kudhibiti ongezeko la mifugo kwa kuiandikisha
ili mgogoro uliopo baina ya hifadhi na wananchi uweze kupatiwa ufumbuzi
kwa kujenga hoja madhubuti.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais anayeshughulikia masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. January
Makamba hii leo ameendelea na ziara ya kukagua hali ya mazingira katika
Mikoa 10 hapa nchini ambapo leo ni siku ya 13. Waziri Makamba pia
atatembelea Mkoa wa Tabora.
Post a Comment