UMOJA
wa Mataifa nchini Tanzania unaendelea na uelimishaji wa wananchi kuhusu
malengo ya Dunia yaliyoelezwa katika Maendeleo Endelevu (SDGs), malengo
ambayo sasa yana takribani mwaka mmoja.
Ili
kuweza kufikisha malengo hayo kila mahali , Umoja wa Mataifa kwa
kushirikiana na serikali utatumia wiki ya vijana kufundisha wanafunzi
400 kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Simiyu ili wawe wakufunzi kwa
wenzao.
Mafunzo
hayo yamelenga kuwafanya vijana kuelewa na kuongeza ufahamu kuhusiana
na malengo hayo ya dunia, hivyo kuwasaidia wenzao na wananchi wengine
kutambua wajibu wao katika utekelezaji wake.
Mafunzo
hayo mkoani Simiyu ni mwendelezo wa mafunzo yaliyozinduliwa mkoani
Arusha na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro
Rodriguez.
Hadi
sasa Umoja wa Mataifa umewezesha vijana 70 kutambua malengo hayo na
kutumika kufunza wengine. Aidha wabunge zaidi ya 180 walipewa mafunzo
hayo huku wahadhiri na wanafunzi 1,000 kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma
(UDOM) wakiwa nao wamenolewa kuhusiana na malengo hayo ya maendeleo
endelevu.
Afisa
Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo
akielezea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mashirika ya Umoja huo
hapa nchini kwenye mafunzo ya siku moja ya Malengo ya Maendeleo Endelevu
(SDGs) kwa vijana wa mkoa wa Simiyu, yaliyofanyika katika ukumbi wa
shule ya Alliance mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Mkurugenzi
Msaidizi, Wizara ya Fedha na Mipango anayeshughulikia umaskini, sera na
uchambuzi, Bw. Mudith Cheyo alichangia katika mafunzo hayo kwa kueleza
ni kwa namna gani serikali inatekeleza malengo hayo ya dunia. Bw. Cheyo
amesema “Asilimia kubwa ya nguvukazi ya taifa letu ni vijana hivyo basi
ni muhimu sana kuwashirikisha katika utekelezaji wa Malengo Ya Dunia
katika ngazi ya taifa. Asilimia 34 ya nguvu kazi ni vijana, serikali
imepanga mikakati kuhakikisha vijana wanapewa uwezo wa kuwawezesha
kuzitumia fursa zilizopo kuleta maendeleo.”
Alisema
kwamba kuwafunza vijana kuhusu malengo hayo ya maendeleo endelevu ni
sehemu ya utendaji wa serikali katika utekelezaji wa malengo.
Akizungumza
katika semina ya malengo endelevu, Bw.Amon Manyama, Mtaalamu wa Umoja
wa Mataifa kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja huo(UNDP), alisema
ajenda ya maendeleo kuelekea mwaka 2030 inahitaji ushiriki wa kila mmoja
wetu hasa vijana.
Ofisa
wa Mawasiliano na Ushirikiano NUNV kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Didi Nafisa akitoa utangulizi wa
Malengo ya Dunia (Global Goals) kwa kundi la vijana wa Simiyu (hawapo
pichani) katika mafunzo ya siku moja yaliyofanyika kwenye ukumbi wa
shule ya Alliance mjini Bariadi mkoani Simiyu.
“Ni
muhimu sana kwa vijana kuelewa Malengo ya Dunia. Huu ni wakati wao. Kwa
kuyaelewa malengo haya inrahisisha utekelezaji wake. Nimefurahi kuona
muamko wa vijana waliojitekeza hapa leo na natumaini watawafikishia
wengine ujumbe huu.” alisema na kuwapongeza vijana hao 400 kwa ushiriki
wao katika kujifunza na kuelewa malengo hayo ya dunia na wajibu wa kila
mmoja wetu.
Septemba 2015, viongozi 193 kutoka nchi mbalimbali duniani walikubaliana kuhusu malengo endelevu 17 kuelekea mwaka 2030.
Mkuu
wa Programu, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon
Manyama akiwapiga msasa wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) vijana
wa mkoa wa Simiyu wakati wa mafunzo ya siku moja yaliyofanyika kwenye
ukumbi wa shule ya Alliance mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Malengo
hayo ambayo yanatakiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 14 ijayo
yanaleta kwa pamoja shughuli za kijamii, kiuchumi na kimazingira ili
kuwa na maendeleo endelevu.
Mashirika
ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania yakifanya kazi chini ya mwavuli
mmoja yanasaidia serikali ya Tanzania katika kuhakikisha kwamba
inafanikiwa katika kuyaingiza malengo yote 17 katika mpango wake wa
maendeleo wa mwaka 2025 kupitia mpango wake wa kuisaidia Tanzania (UNDAP
ll) ulioanza mwaka huu hadi mwaka 2021. Kwa bahati UNDAP II unaenda
sanjari na mpango wa taifa wa maendeleo wa miaka mitano wa 2016-2021.
(FYDP II)
Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya kuondoa Umaskini wa Wizara ya Fedha na Mipango,
Mudith Cheyo akieleza ni namna gani serikali inatekeleza Malengo ya
Dunia na kuwata vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa kuyaelewa vyema na
kuwa mabalozi kwa jamii zao na vijana wenzao ili utekelezaji wa malengo
hayo yafanikiwe kwenye mafunzo ya siku moja kwa vijana wa mkoa wa
Simiyu yaliyofanyika katika ukumbi wa shule ya Alliance mjini Bariadi
mkoani Simiyu.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya kuondoa Umaskini wa Wizara ya Fedha na Mipango, Mudith Cheyo akisisitiza jambo kwenye mafunzo.
Pichani
juu na chini ni umati wa vijana wa Simiyu uliohudhuria mafunzo ya siku
moja ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yaliyoandaliwa na Ofisi ya
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na kufanyika katika
ukumbi wa shule ya Alliance mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Afisa
Ardhi Mtathmini kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu, Lazaro Magumba,
akiuliza swali kwa wawezeshaji kutoka Serikalini na Umoja wa Mataifa
(hawapo pichani) wakati wa mafunzo ya siku moja ya Malengo ya Maendeleo
Endelevu (SDGs) kwa vijana wa mkoa wa Simiyu yaliyoandaliwa na Ofisi ya
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya UN na kufanyika katika ukumbi wa shule ya
Alliance mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Mwalimu
wa Shule ya Sekondari Guduwi Bariadi, Seif Masoud akishiriki kwenye
mafunzo ya siku moja ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa vijana
wa mkoa wa Simiyu yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika
ya UN na kufanyika katika ukumbi wa shule ya Alliance mjini Bariadi
mkoani Simiyu.
Mkuu
wa Programu, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon
Manyama akijibu maswali yaliyoulizwa na washiriki mafunzo ya siku moja
ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa vijana wa mkoa wa Simiyu
yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya UN na kufanyika
katika ukumbi wa shule ya Alliance mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Mwanafunzi
wa SAUT-Mwanza Hatibu Hamisi ambaye pia ni mwanachama wa Asasi ya
Vijana ya Umoja wa Mataifa (YUNA) akieleza vijana wenzake (hawapo
pichani) juhudi na maarifa aliyotumia kutunga kitabu cha ‘Wanawake na
Haki Zao’ ambacho anapanga kutokiuza bali kielimishe jamii ya Watanzania
kuhusu haki za msingi za wanawake wakati mafunzo ya siku moja ya
Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa vijana wa mkoa wa Simiyu
yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya UN na kufanyika
katika ukumbi wa shule ya Alliance mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Mwanafunzi
wa SAUT-Mwanza Hatibu Hamisi (kushoto) ambaye pia ni mwanachama wa
Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa (YUNA), akikabidhi kitabu hicho kwa
Mkuu wa Programu, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon
Manyama katika mafunzo ya siku moja kwa vijana wa Simiyu yaliyofanyika
kwenye ukumbi wa shule ya Alliance mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Ofisa
wa Mawasiliano na Ushirikiano NUNV kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Didi Nafisa (kulia) akibadilishana
mawazo na Katibu Mkuu Mtendaji wa Shirikisho la Vyuo Vikuu, Zenda
Daniel wakati wa mafunzo ya siku moja ya Malengo ya Maendeleo Endelevu
(SDGs) kwa vijana wa mkoa wa Simiyu yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya UN na kufanyika katika ukumbi wa shule ya Alliance
mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Mchekeshaji
maarufu wa mkoa wa Simiyu anayefahamika kwa jina la Madodoso a.k.a
Handsome boy wa Simiyu akitoa burudani kwa vijana wakati wa mafunzo ya
siku moja ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa vijana wa mkoa wa
Simiyu yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya UN na
kufanyika katika ukumbi wa shule ya Alliance mjini Bariadi mkoani
Simiyu.
Mchekeshaji
maarufu wa mkoa wa Simiyu anayefahamika kwa jina la Madodoso a.k.a
Handsome boy wa Simiyu (kulia) akimvunja mbavu Mkuu wa Programu, Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama alipokuwa akitoa
burudani kwa washiriki wa mafunzo ya siku moja ya Malengo ya Maendeleo
Endelevu (SDGs) kwa vijana wa mkoa wa Simiyu yaliyofanyika katika ukumbi
wa shule ya Alliance mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Vijana wakiangua vicheko ukumbini hapo.
Sehemu ya washiriki wakiwemo walimu wa shule mbalimbali walioambatana na wanafunzi wao.
Baadhi
ya vijana katika picha ya pamoja na mabango ya malengo ya dunia mara
baada ya kumalizika kwa mafunzo ya siku moja ya Malengo ya Maendeleo
Endelevu (SDGs) kwa vijana wa mkoa wa Simiyu.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa waliokuwa mkoani Simiyu kwenye
maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa katika picha ya pamoja
wakiwakilisha malengo ya dunia.
Post a Comment