Wanafunzi wa Shule ya Msingi
Mlandege iliyo katika Manispaa ya Iringa, wakishirikiana na Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January
Makamba katika Kampeni ya Upandaji miti Shuleni hapo.
Hali halisi ya Mto Ruaha kwa
sasa, kina cha maji kimeshuka sana na kusabisha vifo kwa baadhi ya
wanyama wanaotegeme Mto huo. Upungufu wa kina hicho unatokana na
shughuli za kibinadamu pembeni mwa mto huo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akiwa na watendaji
kutoka shamba la Umwagiliaji la Madibila ambapo inasemekana maji mengi
yanapotea hivyo kuadhiri mtiririko wa maji katika mto Ruaha Mkuu.
……………………………………………………………….
NA Lulu Mussa- Mbarali
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais mwenye dhamana ya kusimamia Muungano na Mazingira Mheshimiwa
January Makamba ameshiriki katika zoezi la kupanda miti katika Shule
Msingi Mlandege katika Manispaa ya Iringa Mjini.
Waziri Makamba amesema kuwa suala
la kupanda miti ni agenda ya kitaifa sasa na kuanzia mwakani kwa
kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,
Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari wanapo ripoti mashuleni ni
lazima aje na miti ili ndipo apokelewe.
“Ndugu zangu wana Iringa,
tumeazimia kupanda miti kwa wingi ili kunusuru nchi yetu kuwa jangwa,
maana tafiti zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia sitini na moja (61) ya
nchi yetu ni inatishia kuwa jangwa, hivyo ni wajibu wetu kunusuru hali
hii” Makamba alisisitiza.
Waziri Makamba pia alitoa onyo
kwa wachafuzi wa chanzo cha maji cha Mto Ruaha ikiwa ni pamoja na jamii
zinazofanya shughuli za kilimo, ufyatuaji wa matofali na ujenzi
pembezoni mwa mto huo kuondolewa na kwa wale watakaokaidi kushtakiwa
mara moja na kuahidi kurudi tena kufuatilia utekelezaji wa agizo hilo.
kwa upande mwingine Waziri
Makamba ametembelea Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na kujionea upungufu wa
maji kwa kiwango kikubwa katika Mto Huo. Kaimu Mhifadhi wa Hifadhi ya
Ruaha Bw. Moronda B. Moronda amebainisha kuwa upungufu huo si tu una
athari kwa wanyama bali ikolojia nzima ya eneo hilo, na kubainisha kuwa
kilimo cha umwagiliaji katika mashamba ya Mbarali ni chanzo kikuu cha
tatizo hilo.
kufuatia taarifa hiyo, Waziri
Makamba alitembelea mashamba makubwa ya Mpunga na kuagiza kufanyika kwa
Ukaguzi wa mazingira kwa kuwa suala hilo ni la kisheria kwa mujibu wa
sheria ya Mazingira ya mwaka 2004.
Pili, Waziri Makamba ameagiza
kuundwa kwa kikosi kazi kitakachojumuisha wajumbe kutoka Mikoa ya Mbeya,
Songwe, Iringa, Dodoma, Morogoro na wadau wa mazingira ili kubaini hasa
chanzo cha tatizo hilo ili kupata ufumbuzi wa haraka.
Waziri Makamba anaendelea na ziara yake ya kikazi ya kukagua hali ya mazingira nchini, hii leo amewasili katika Mkoa wa Njombe.
Post a Comment