Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
ahutubia wananchi wa wilaya ya Nachingwea katika kiwanja cha Sokoine
waziri mkuu alipokea malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusiana na
biashara ya korosho Ikamlazimu waziri mkuu kumuagiaza Waziri wa kilimo
afanye mapitio makini kweznye bodi nzima ya korosho
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
apokea hundi ya mfano ya zaidi shilingi milioni kumi nasita kutoka kwa
Mkuu wa Mkoa walindi kwa ajili ya Rambirambi kwa wananchi wa mkoa wa
Kagera kulia kwa waziri mkuu ni mkewe Mary Majaliwa waziri mkuu yupo
mkoani Lindi katika ziara ya kikazi katika wilaya ya Nachingwea na
Ruwangwa
Picha na Chris Mfinanga
………………………………………………………………………………………………..
*Aagiza ifanyiwe marekebisho makubwa
*Aishangaa kung’ang’ania minada
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amemuagiza Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba
kuifanyia marekebisho makubwa Bodi ya Korosho na menejimenti yake baada
ya kushindwa kusimamia zao hilo ipasavyo.
Amesema Serikali itafanya mapitio
ya bodi zote za mazao ya biashara na imeanza na zao la korosho kisha
zao la pamba, tumbaku, kahawa, katani na chai. Katika tathmini na
mapitio hayo , bodi itakayobainika kushindwa kutekeleza majukumu yake
itavunjwa.
Waziri Mkuu alitoa agizo hilo
jana jioni (Jumapili, Oktoba 16, 2016) wakati akihutubia wananchi katika
mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja cha Sokoine wilayani
Nachingwea mkoani Lindi.
Alisema anaishangaa bodi hiyo
kuacha kutekeleza majukumu yake na kuingilia minada ya korosho na kuzuia
baadhi ya wafanyabiashara wasiweze kununua zao hilo hali inayoashiria
kuwepo kwa watu waliopangwa kununua bila ya kufuata utaratibu.
“Bodi leo wamejipa jukumu la
kusimamia minada ! sio kazi yao ni kazi ya chama kikuu, zao la korosho
linalimwa kutoka mkoani Ruvuma hadi Tanga, mtasimamia minada mingapi
viachieni vyama vikuu. Vyama vikuu vikiharibu walalamikaji waje kwenu
kama sehemu ya rufaa. Sasa nyinyi mnasimamia minada mnaharibu
walalamikaji watakwenda kwa nani ? kwa nini mng’ang’anie kwenda kwenye
minada,” alihoji Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu alisema Ijumaa
(Oktoba 14,2016) bodi hiyo ilisitisha mnada wa korosho Lindi kwa sababu
wanunuzi hawakuweka bondi (dhamana ya mauzo) na alishatoa maagizo ya
kuwataka wanunuzi wasiruhusiwe kununua hadi waweke asilimia 25 ya
malipo.
Alisema maagizo hayo aliyatoa
tangu mwezi Aprili ila watendaji wa bodi hiyo hawakuyafanyia kazi kwa
wakati na badala yake waliwazuia wafanyabiashara waliotaka kununua
korosho Lindi kwa madai ya kutokuwa na bondi huku wakiwaruhusu wa
Mtwara.
“Kama kule walinunua bila bondi
kwa nini wasiwaruhusu na Lindi wakanunua bila bondi ili nijue kwamba
mliamua kugoma kuteleza maelekezo ya Serikali? Au hamkumtaka aliyeshinda
nyie mlikuwa mnamtaka nani nitashughulika na nyie,” alisisitiza.
Aliongeza kuwa “Nimesema tukitoa
maelekezo lazima yatekelezwe na atakayeshindwa hatufai, Mheshimiwa
mbunge umelalamika juu ya bodi hawa ndio wabeba maelekezo hatujawahi
kuona bodi ya korosho ikienda vijijini kuzungumza na vyama vikuu hata
mara moja,”.
Akizungumzia kuhusu suala la
wakulima kulazimishwa kufungua akaunti za kupitishia malipo yao alisema
wasiwalazimishe.“Waelimisheni wakulima umuhimu wa kufungua akaunti
lakini si kwa kuwalazimisha wote wawe na akaunti hadi yule mwenye kilo
tano…na akaunti yenyewe inafunguliwa kwa sh. 100,000,” alisema.
Alisema “’wanashindwa kutekeleza
niliyowaagiza, halafu wanasingizia utendaji wao mbovu kuwa ndio maagizo
yangu,’ niliwaagiza wapi,” alihoji na kuongeza kuwa “yapo makundi
yanafanya mambo yanavyotaka alafu yakiwazidi mambo wanasingizia viongozi
wajuu na ndio wale wanaosema kila kitu nimeagizwa kutoka juu, juu wapi?
“Lazima tuendelee kudhibiti
nidhamu ya vyombo vya tunavyoviunda kwa ajili ya kuwahudumia wananchi.
Tutaendelea kusimamia nidhamu kwa taasisi zinazowahudumia wakulima nchi
nzima,” alisisitiza.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa
Lindi, Bw. Godfrey Zambi alimkabidhi Waziri Mkuu msaada wa sh. milioni
16.3 pamoja na nguo kwa ajili ya kusaidia wananchi walioathirika na
tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Jumamosi, Septemba 10, mwaka
huu na kusababisha vifo vya watu 17 na wengine 440 walijeruhiwa.
Post a Comment