Naibu
Waziri (Ofisi ya Waziri Mkuu), Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na
Walemavu, Dkt. Abdallah Possi amelipongeza Shirika la Umoja wa Mataifa
la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) kwa kusaidia kutoa elimu kwa
wananchi kuhusu watu wenye ualbino pamoja na kufanya tathmini jinsi
wananchi walivyo na uelewa kuhusu watu hao.
Dk. Possi ameyasema hayo katika
mkutano wa kuelezea tathmini ambayo imefanywa na UNESCO kwa wananchi wa
wilaya nne ambazo tathmini ilifanyika na kusema kuwa ni jambo zuri
ambalo limesaidia kuonyesha hali jinsi ilivyo na ni njia gani ambayo
serikali inaweza kutumia ili kumaliza vitendo vya ukatili kwa watu wenye
ualbino.
“Watu wenye ualbino wamekuwa
wakiteseka kwa kipindi kirefu, wanakosa nafasi ya kusoma, kufanya
biashara na mambo mengi yanawakabili, watu wa mashirika sio suluhisho ni
jamii yenyewe, watu wengi bado hawana elimu ya kutosha kuhusu ualbino,
“Inabidi ifike hatua watu wenye
ualbino waishi sawa na watu wengine na serikali imekuwa ikifanya
jitihada kumaliza vitendo hivyo lakini inabidi jamii itambue hili sio
jukumu la serikali peke yake ni muhimu kila mmoja akashiriki
kuvitokomeza vitendo vya ukatili, UNESCO imetuonyesha njia ya kuiwezesha
serikali kufanikisha nia yake,” alisema Dkt. Possi.
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa
UNESCO nchini, Zulmira Rodrigues akizungumza machache kabla ya
kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,
Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi kutoa hotuba
kwenye mkutano wa UNESCO unaoangalia tathmini ya watu wenye ulemavu wa
ngozi uliofanyika leo katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es
Salaam. (Habari picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Kwa upande wa UNESCO kupitia
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Zulmira Rodrigues alisema
UNESCO imnatambua kila mwanadamu ana haki ya kuishi kama binadamu
wengine na kupitia utafiti wao ambao uliambatana na kutoa elimu
wanaamini kuwa ni muda wa jamii kushirikiana ili kutokomeza vitendo vya
kikatili kwa maalbino.
“UNESCO imeamua kujihusisha
sana na hili jambo na kujitahidi kutoa elimu kwa jamii, tumeanza
kulifanyia kazi jambo hili la kikatili kwa maalbino na mashambulizi
ambayo wamekuwa wanakutana nayo sababu ya imani za kishirikina ambazo ni
kinyume na haki za kibinadamu,
“Utafiti huu utaweza kusidia
kumaliza vitendo vya kikatili kwa watu wenye ualbino, kila mtu ana haki
za kimsingi na hilo ndilo ambalo UNESCO inalisimamia, na katika
kufanikisha hili kila mtu katika jamii kwa nafasi yake ana wajibu wa
kushiriki kumaliza vitendo hivi, ni lazima kushirikiana kumaliza jambo
hili,” alisema Rodrigues.
Tathmini hiyo imefanyika katika
wilaya nne ambazo ni Misungwi na Sengerema kwa Mwanza, Msalala iliyopo
Shinyanga na Bariadi mkoani Simiyu.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera,Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah
Possi akizungumza katika mkutano wa UNESCO unaoangalia tathmini ya watu
wenye ulemavu wa ngozi uliofanyika leo katika hoteli ya Protea Courtyard
jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya watu
wenye Alibinism Tanzania (TAS) Nemes Temba akitoa neno kwenye mkutano wa
UNESCO unaoangalia tathmini ya watu wenye ulemavu wa ngozi uliofanyika
leo katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam na kiongozi mkuu wa tathmini hiyo, Dkt. Nandera Mhando akiainisha
mambo muhimu yaliyobainika kwenye tathmini wakati mkutano wa UNESCO
unaoangalia tathmini ya watu wenye ulemavu wa ngozi uliofanyika leo
katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Sweden nchini
Tanzania Bi. Katarina Rangnitt akitoa maoni kwenye mkutano wa UNESCO
unaoangalia tathmini ya watu wenye ulemavu wa ngozi uliofanyika leo
katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Kulia ni Balozi
wa Uturuki nchini, Yasemin Eralp.
Balozi wa Uturuki nchini,
Yasemin Eralp akizungumza jambo kwenye mkutano wa UNESCO unaoangalia
tathmini ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinism) uliofanyika leo
katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la
Uhamiaji (IOM) nchini, Dr. Qasim Sufi akifafanua jambo wakati wa
mkutano wa UNESCO unaoangalia tathmini ya watu wenye ulemavu wa ngozi
(Albinism) uliofanyika leo katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar
es Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Mhe. Dkt. Abdallah
Possi akifafanua jambo kwenye mkutano wa UNESCO unaoangalia tathmini ya
watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinism) uliofanyika leo katika hoteli ya
Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Picha juu na chini ni Sehemu ya
washiriki wa mkutano wa UNESCO unaoangalia tathmini ya watu wenye
ulemavu wa ngozi (Albinism) wakiwemo wadau kutoka mashirika na taasisi
mbalimbali uliofanyika leo katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar
es Salaam.
Mshehereshaji wa mkutano wa
UNESCO unaoangalia tathmini ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinism),
Mathias Herman akiendesha mjadala kwa washiriki katika mkutano huo
uliofanyika leo katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Mhe. Dkt. Abdallah
Possi akibadilishana mawazo na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Bi.
Katarina Rangnitt (wa pili kushoto), Balozi wa Uturuki nchini, Yasemin
Eralp (wa pili kulia) pamoja na Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji
(IOM) nchini, Dr. Qasim Sufi wakati wakijiandaa na zoezi la picha ya
pamoja.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Mhe. Dkt. Abdallah
Possi katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa UNESCO
unaoangalia tathmini ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinism)
uliofanyika leo katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Check Also
WAZIRI MKUU NA MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI DODOMA LEO
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum Mary Mwanjelwa kwenye viwanja vya …Leave a Reply
Your email address will not be published. Required fields are marked *