Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia wakazi wa kijiji cha Nsola ambapo alikagua miradi mbali mbali
ya ufugaji samaki ikiwa sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akikagua shamba la kilimo cha kisasa Greenhouse (Bandakitalu) la
Ngongoseke lililopo kijiji cha Nsola wilayani Magu mkoa wa Mwanza
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akimsikiliza kwa makini mwanafunzi Evodia Anatori wa shule ya sekondari
ya kata ya Idetemya akionyesha kwa vitendo namna ya kuchanganya kemikali
kwenye maabara ya shule hiyo iliyopo wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwapungia wananchi wa Idetemya mara baada ya kufungua bweni la
wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari ya kata ya Idetemya wilayani
Misungwi mkoani Mwanza.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwasalimia wananchi waliojitokeza kwa wingi kumsalimia kwenye maeneo ya Nyakato mkoani Mwanza.
………………………………………………..
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwasalimia wananchi waliojitokeza kwa wingi kumsalimia kwenye maeneo ya Nyakato mkoani Mwanza.
………………………………………………..
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
amewaagiza viongozi mkoa wa Mwanza kuimarisha maradufu doria katika Ziwa
Victoria kama hatua ya kukabiliana na tatizo la uvuvi haramu ambao
umepunguza kwa kiasi kikubwa samaki kwenye ziwa hilo
Rais ametoa maagiza hayo katika mikutano ya hadhara aliyoifanya katika wilaya za Kwimba, Misungwi na Magu mkoani Mwanza katika ziara yake ya kikazi ambayo imeigia siku ya PILI mkoani humo.
Makamu
wa Rais amewataka viongozi hao kuwachukulia hatua kali za kisheria watu
watakaokamatwa wakivua kwa zana haramu ua kwa sumu ili kukomesha tatizo
hilo katika Ziwa Victoria.
Ameonya
kuwa wavuvi haramu wakiachwa waendelee kufanya uvuvi huo wataharibu
ziwa lote hasa mazalia ya samaki hali ambayo itasababisha viwanda wa
kusindika samaki mkoani humo kufungwa na mamia ya watu kukosa ajira
kutokana na shughuli za
uvuvi.
uvuvi.
Akizindua
na kuweka mawe ya msingi kweye mabweni ya wanafunzi wasichana katika
shule za sekondari ya Idetemya wilayani Misungwi na shule ya Sekondari
ya Archbishop Anthony Mayala wilayani Kwimba, Makamu wa Rais amepongeza
juhudi za viongozi wa mkoa wa Mwanza na wadau wa maendeleo kwa kujenga
mabweni hayo ambayo yatasaidia wasichana kuondokana na mazingira
hatarishi ikiwemo kupata
mimba.
mimba.
Makamu
wa Rais amewaagiza wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wa
Halmashauri nchini kuweka mikakati madhubuti ya kujenga mabweni ya
wasichana kama hatua ya kukabiliana na tatizo la wanafunzi kupata mimba
na kuacha shule.
Akisalimia
mamia ya wananchi wa maeneo ya Igoma na Nyakato jijini Mwanza
waliojitokeza barabarani ili kumsalimia, Makamu wa Rais Samia Suluhu
Hassan amewahakikishia wananchi hao kuwa ahadi zote zilizotolewa na
viongozi hao wakati wa kampeni zitatekelezwa ikiwemo tatizo la ajira kwa
vijana.
Amewahimiza
wananchi waunge mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano katika
kubaini walarushwa na watendaji wanaohujumu miradi ya maendeleo ili
wachukuliwe hatua za kisheria.
Amesisitiza
kuwa serikali ya awamu ya tano inataka kuona rasilimali zilizopo nchini
zinatumika vizuri kwa ajili ya manufaa ya wananchi wote na sio kwa
idadi ya watu wachache.
Akiwa
mkoani Mwanza Makamu wa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Samia Suluhu Hassan amekagua,kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika
miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi katika
mikutano ya hadhara na kuwaeleza mipango ya mikakati ya serikali ya
awamu ya Tano ya kuwaletea wananchi hao maendeleo.
Katika
hatua nyingine, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amechangia mabati
100 na mifuko ya saruji 100 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa mabweni ya
wanafunzi katika shule ya sekondari ya wasichana ya Archbishop Anthony
Mayala wilayani Kwimba mkoani Mwanza.
Post a Comment