Aligunduliwa kuwa na virusi vya HIV mwaka 1997
Princes
Kasune ni mmoja ya wanaharakati maarufu wa ugonjwa wa ukimwi nchini
Zambia na alichaguliwa kama mbunge wa upinzani mwezi Agosti.Aligunduliwa
kuwa na virusi vya HIV mwaka 1997 na mwaka uliofuatia alitangaza
hadharani hali yake kinyume na mapenzi ya mmewe na tamaduni kwa kufanya
hivyo.
“Wakati
niligundua kuwa nilikuwa na virusi vya HIV, nilijua kuwa nilikuwa na
jukumu la kueneza habari kuhusu njia HIV unaweza kuambukizwa, unaweza
kuzuiwa na pia njia za kumaliza unyanyapaa,” Kasume mwenye umri wa miaka
40 aliiambia BBC.
Katika
sehemu kubwa ya maisha yake, amethirika na virusi vya HIV. Alilelewa
kijijini na aliwapoteza wazazi wake wote kwa ugonjwa wa ukimwi akiwa na
umri wa miaka 14 na kisha akaolewa akiwa na umri wa miaka 18.
Anasema ana ana jukumu la kueneza habari kuhusu njia HIV unaweza kuambukizwa, unaweza kuzuiwa na pia njia za kumaliza unyanyapaa
Akiwa
na ndoto na kuona kizazi kichajo kisicho na virusi vya ukimwi, uamuzi
wake wa kutangaza hadharani hali yake ulizua tofauti kubwa.
Kanisa
lake lilimtimua kwa kuchukua hatua hiyo na kwa kwenda kinyume na
matakwa ya mmewe kuhusu kuweka siri hali yake ya kuishi na virusi vya
ukimwi.
Amesafiri
sehemu mbali mbali za dunia na kukutana na viongozi wakiwemo marais wa
zamani nchini Marekani wakiwemo Bill Clinton na George W Bush pamoja na
katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.
Wakati mmoja akitoa hotuba, aliwakumbusha wabunge wenzake kuhusu umuhimu wa kupimwa hali zao.
Post a Comment