MFUGAJI na mkazi wa kijiji cha Kagera
wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Majibwa Magesa ameuawa baada ya kuvamiwa
na watu wasiojulikana wanaotuhumiwa kuwa ni majambazi.
Diwani wa Kata ya Kagera Nkanda, Ezekiel Mshingo amewaambia waandishi wa habari kwamba Magesa aliuawa usiku wa kuamkia jana majira ya saa nane usiku.
Mshingo alisema kuwa Magesa aliuawa baada ya kupigwa risasi katika makalio akiwa katika harakati za kujiokoa.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba watu hao walikuwa wezi.
Kamanda Mtui alisema kuwa hadi sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo ingawa wapo watu wanaoshukiwa kuhusika na sasa wamekimbia na polisi inaendelea na upelelezi wa tukio hilo.
Imeandikwa na Fadhili Abdallah, Kigoma

Post a Comment