Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa pamoja na kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani humo wamefanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo katika halmasahuri hiyo .
Ziara hiyo iliambatana na ukaguzi wa Scheme ya umwagiloaji ya Ifumbo ambapo katika mradi huo kuna zaidi ya hekta 1,000 (alfu moja) zinazotumia scheme hiyo. Mara baada ya kutembelea Scheme hiyo Mkuu huyo wa Wilaya ameonesha kulidhishwa na namna ambavyo wananchi wanatumia fursa hiyo katika kujiongezea kipato chao .
Amesema Wananchi wa Ifumbo wanatumia kwa mazao mbalimbali yakiwemo mahindi, ufuta, kunde, mtama, alizeti, kunde pamoja na matunda.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya pamoja na Kamati hiyo ya Ulinzi na Usalama wamebaini kuwepo kwa changamoto kubwa ya maeneo katika mradi huo wa umwagiliwaji kukodishwa kwa watu wengine badala ya wananchi wenyewe kulitumia eneo hilo kwa ajili ya kilimo huku hekta 100 tu kati ya 1000 ndizo zinazolimwa .
Kutokana na hali hiyo Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wananchi hao kuhakikisha wanaongeza kiwango cha Kilimo kwa kuongeza mazao kama viazi lishe ambayo yatawasaidia katika kupunguza tatizo la macho kutokana na uwingi wa vitamin A iliyomo katika viazi.
Pia ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi hao kutekeleze mpango wa ufyatuaji tofali kwa kila Kitongoji kwa ajili ya ujenzi wa zahanati na matundu ya vyoo
Post a Comment