Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akifurahia jambo na moja wa vijana wa Skauti eneo la Visakazi alipotembelea jimboni humo. |
Mwenyekiti wa Chama cha CCM Tawi la Visakazi akieleza baadhi ya malalamiko ya wananchi mbele ya Mbunge wao Ridhiwani Kikwete hayupo pichani kwenye ofisi ya chama hicho katika mkutano. |
Wananchi
katika jimbo la Chalinze mkoani Pwani, wamekiri kuona mwanga kwa jinsi
viongozi wanavyotatua matatizo yao, kufuatia kuongezeka kwa
ushirikishwaji wa wananchi katika kutoa kero zao mbele za viongozi na
kujadiliana utatuzi wake kwa pamoja.
Kauli
hiyo imetolewa wakati wa mkutano kati ya wananchi wa kitongoji cha
Visakazi kata ya Ubena Chalinze na Mbunge wa Chalinze RIDHIWANI KIKWETE,
ambapo sehemu kubwa ya wananchi waliohojiwa wameonyesha kukubali kwamba
mikutano ya majadiliano mara kwa mara kati ya viongozi na wananchi
huongeza ufanisi katika utendaji.
Naye
Mbunge wa Chalinze kwa upande wake amebainisha kuwa mikutano hiyo ni
sehemu ya utaratibu wa kiuongozi ambao amejiwekea katika kuhakikisha
anatatua kero za wananchi wake kwa wakati muafaka na kwa kiwango
kinachotakiwa.
Wakati
wa mkutano huo, wananchi hao wameshukuru kwa kazi kubwa ambazo tayari
zimefanyika katika jimbo hilo ikiwemo uimarishaji wa huduma za afya,
elimu na pamoja na mambo mengine ya kijamii.
“Mbunge
huyu amekuja na staili kama ya wakati wa mzee wake wananchi tunapewa
nafasi tunasema hata yetu binafsi naamini hii itasaidia sana na utakuwa
karibu na wananchi wako”, alisema Bi Semeni Masound,
Aidha wameelezea kuridhishwa na juhudi zinazoendelea kuchukuliwa katika kutatua migogoro kati ya wakulima na wafugaji.
katika
hatua nyingine Mbunge Ridhiwani ameshiriki katika mazishi ya Mama mzazi
wa Diwani wa zamani Kata ya Bwilingu Ndg.Rashidi Shomari Lugazo.
Mbunge huyo ataendelea na ziara ya kutembelea wananchi tarehe 5 novemba.
Post a Comment