Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This



1-1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, kesho tarehe 04 Novemba, 2016 atafanya mahojiano ya kwanza na waandishi wa habari tangu aingie madarakani mwaka mmoja uliopita.
Mahojiano haya yatarushwa moja kwa moja na vituo vya habari vya redio na televisheni kutoka ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam na yataanza saa 4:00 asubuhi.
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais inapenda kuwaalika wananchi wote kusikiliza na kutazama mahojiano hayo ili mpate fursa ya kujua mambo mbalimbali ambayo Mheshimiwa Rais atayatolea majibu.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top