Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, ambapo aliwaasa wananchi kuchukua uamuzi wa kupima afya zao na kupatiwa matibatu. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume hiyo, Dk. Hedwiga Swai.
Na Dotto Mwaibale
WANANCHI wametakiwa kupima kila wakati na kuendelea kutumia kinga ili kujiepusha na maambuki mapya ya VVU.
Mwito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko katika kikao cha makamishina wapya wa tume hiyo kilichoketi jijini Dar es Salaam juzi.
"Tunapaswa kuwa ni mikakati endelevu ya kupambana na ugonjwa wa ukimwi kwani bado kunachangamoto kubwa" alisema Maboko.
Maboko alisema watanzania wasidanganyike kuwa ukimwi umekwisha ugonjwa huo bado upo na ni changamoto kubwa.
Alisema changamoto kubwa ya ugonjwa huo bado ipo katika baadhi ya mikoa hasa ile ya nyanda za juu kama Iringa na Njombe hivyo wananchi wasibweteke kuwa ugonjwa huo umekwisha.
Alisema kwa Tanzania Bara kunamaambukizi ya asilimia 5.3 sawa na watu milioni mbili waliopata maambukizi.
Post a Comment