Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akitoa heshima za mwisho kwa Spika Mstaafu, Samuel Sitta, bungeni mjini
Dodoma, Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiweka shada la maua kwenye jeneza la Spika Mstaafu Samwel Sitta,
bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Mstaafu, Samuel
Malecela akimpa pole mjane wa Spika Mstaafu, Margareth Sitta bungeni
mjini Dodoma Novemba 11, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akimfariji mjane wa Spika Mstaafu Mama Margareth Sitta baada ya mwili
wa Spika Mstaafu, Marehemu Samuel Sita kuwasili kwenye uwanja wa ndege
wa Dodoma Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary
Majaliwa (wapili kulia) akimfariji mjane wa Spika Mstaafu Mama
Margareth Sitta baada ya mwili wa Spika Mstaafu, Marehemu Samuel Sita
kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Novemba 11, 2016. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza katika kikao maalum cha bunge cha kumuenzi Spika Mstaafu,
Samuel Sitta, bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Mwili wa Spika Mstaafu, Samuel Sitta ukiingizwa bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Mwili wa Spika Mstaafu Samuel
Sitta ukiteremshwa kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Novemba 11, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
Spika wa Bunge, Job Ndugai pamoja na viongozi wengine wakiusubiri mwili
wa Spika mstaafu, Samuel Sitta uteremshwe kwenye ndege katika uwanja wa
ndege wa Dodoma Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
ameongoza mamia ya wabunge, viongozi wa kitaifa na watumishi wa Ofisi ya
Bunge kuuaga mwili wa Spika Mstaafu, Samwel Sitta.
Bw. Sitta alifariki dunia usiku wa kuamkia Novemba 7 katika hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani.
Akizungumza wakati wa kuuaga
mwili huo Bungeni mjini Dodoma leo (Ijumaa, Novemba 11, 2016), Waziri
Mkuu ametoa pole kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai, mke wa
marehemu Mheshimiwa Magreth Sitta, mama wa marehemu Hajat Zuena
Fundikila na familia ya marehemu na wabunge wote.
“Nitumie fursa hii pia kukupa
pole Mheshimiwa Spika kwa pigo ambalo Bunge lako tukufu imelipata kwa
kumpoteza mmoja wa viongozi mahiri wa Bunge hili katika historia ya nchi
yetu. Msiba uliotupata wa Spika Mstaafu wa Bunge la Tisa (2005-2010) na
Mbunge Mstaafu wa jimbo la Urambo mkoani Tabora ni mzito.”
Amesema Bw. Sitta alikuwa mtu
muhimu aliyetoa mchango mkubwa katika uongozi na maendeleo. “Serikali
imepokea taarifa za msiba huu kwa mshtuko mkubwa. Historia ya Mzee Sitta
ni pana sana. Tunatambua utumishi uliotukuka katika nyadhifa mbalimbali
alizozitumikia. Tutamkumbuka kwa utumishi wake,” amesema.
Waziri Mkuu ameongeza kuwa:
“Tuzidi kumuomba Mwenyezi Mungu kila mtu kwa imani yake ili tuweze
kufikia japo mema machache aliyoyatenda katika enzi za uhai wake.”
Enzi za uhai wake Mhe. Sitta
alibahatika kufanya kazi na Marais wa awamu nne zilizopita tangu ya
kwanza ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, akiwa mbunge kwa
miaka 30.
Nyadhifa nyingine alizowahi
kushika ni pamoja na Mkuu wa Mikoa ya Iringa na Kilimanjaro, Waziri wa
Ujenzi, Waziri anayesimamia Ustawishaji Makao Makuu, Waziri wa Katiba na
Sheria, Waziri wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la
Katiba.
Post a Comment