Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(kulia) akizungumza na waandishi wa
habari leo Jijini Dar es Salaam (hawapo pichani)wakati wa hafla ya
kumkabidhi Bendera ya Taifa Bi. Julietha Kabete (kushoto) Mrembo
atakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Afrika 2016 nchini
Nigeria.
Mwakilishi wa Millen Magese
group company Ltd Bw. Matukio Aranyande Chuma(katikati) akitoa maelezo
kuhusu mashindano ya Urembo ya Afrika kwa mwaka 2016 kwa waandishi wa
habari leo Jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa hafla ya
kumkabidhi Bendera ya Taifa Bi. Julietha Kabete(kushoto) Mrembo
atakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Afrika 2016 nchini
Nigeria kulia ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape
Moses Nnauye.
Mwenyekiti wa Kamati ya Miss
Tanzania Bw. Hashim Lundenga ( katikati) akifafanua jambo kwa waandishi
wa habari leo Jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) kuhusu mchakato wa
kumpata mshiriki wa mashindano hayo kutoka kwa washiriki wa Miss
Tanzania 2016 wakati wa hafla ya kumkabidhi Bendera ya Taifa Bi.
Julietha Kabete(kushoto) Mrembo atakayeiwakilisha Tanzania katika
mashindano ya Miss Afrika 2016 nchini Nigeria kulia ni Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye.
Bi. Julietha Kabete(katikati)
akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam wakati wa
hafla ya kukabidhiwa Bendera ya Taifa na Waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(kulia) kwenda kuiwakilisha
Tanzania katika mashindano ya Miss Afrika 2016 yatakayofanyika nchini
Nigeria kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania Bw. Hashim
Lundenga .
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(kulia) akimkabidhi Bendera ya Taifa
Bi. Julietha Kabete(kushoto) Mrembo atakayeiwakilisha Tanzania katika
mashindano ya Miss Afrika 2016 nchini Nigeria.
Baadhi ya waandishi wa habari
wakifuatilia matukio wakati wa hafla ya kumkabidhi Bendera ya Taifa Bi.
Julietha Kabete Mrembo anatakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya
Miss afrika 2016 nchini Nigeria iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari
wakifuatilia matukio wakati wa hafla ya kumkabidhi Bendera ya Taifa Bi.
Julietha Kabete Mrembo anatakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya
Miss afrika 2016 nchini Nigeria iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Bi Julietha Kabete Mrembo
anatakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss afrika 2016
nchini Nigeria iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM.
…………………………………………………..
Na Shamimu Nyaki WHUSM
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ameahidi kuendelea kufanya mageuzi
makubwa katika mashindano ya urembo hapa nchini ili kuondoa dosari
zinazojitokeza katika mashindano hayo.
Mhe. Nape ametoa ahadi hiyo leo
Jijini Dar es Salaam wakati akimkabidhi Bendera Mshiriki wa Tanzania
katika mashindano ya urembo Bara la Afrika kwa mwaka 2016
yatakayofanyika Novemba 28 mwaka huu nchini Nigeria.
Mhe Nnauye ameongeza kuwa lengo
la Serikali ni kuhakikisha kuwa mashindano kama haya yanakuwa na tija
kwa Taifa hasa katika kuleta ajira kwa vijana pamoja na kuitangaza nchi
kimataifa kupitia urembo.
“Serikali nia yake ni
kuhakikisha kuwa jambo hili linakuwa bora, linaminiwa na kuheshimika
hivyo watanzania wote watajivunia uwepo wa mashindano ya urembo nchini”
alisistiza Mhe Nnauye.
Aidha Mwakilishi wa Millen Magese
group Ltd Bw. Matukio Aranyande Chuma amesema kuwa shindano hili
litailetea sifa Tanzania na ni kwa mara ya kwanza kufanyika hivyo
wataitumia fursa hiyo kuitangaza nchi kimataifa kupitia urembo.
“ kwa niaba ya Millen Magese
group Ltd tunatoa shukrani zetu kwa Serikali na Kamati ya Miss Tanzania
kwa kutuunga mkono katika jambo hili na tunaahidi kufanya vizuri katika
mashindano haya”Alisema Bw. Chuma.
Kwa upande wake Mshiriki kutoka
Tanzania anayekwenda kushiriki mashindano hayo Bi. Julietha Kabete
ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuunga mkono mashindano mbalimbali ya
urembo Tanzania inaposhiriki.
“Naahidi kuitangaza nchi yangu
vizuri katika mashindano haya na naomba watanzania waniombee na
wanipigie kura ili niweze kushinda na kuitangaza Tanzania kimataifa
katika urembo” Alisema Bi Julietha.
Mashindano ya Miss Afrika
yameanzishwa mwaka 2016 na Prof. Bena Yage ambaye ni Gavana wa Jimbo la
Cross River nchini Nigeria kwa lengo kupata mabalozi wa nchi za Afrika
watakaosaidia kutangaza na kuelimsha waafrika kuhusu uchumi unaozingatia
utunzaji wa mazingira.
Post a Comment