Mkurugenzi wa Uendeshaji wa kampuni ya Aggrey&Clifford,Cobus van Zly (kulia) na Mkurugenzi wa huduma za Matangazo,Oliver Mutere (katikati) wakikabidhi baadhi ya zawadi kwa watoto wenye mazingira magumu kwenye kituo cha Sadeline kilichopo Mbezi Juu wilayani Kinondoni kwa Msimamizi wa kituo hicho,Sarah Kitainda wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipotembelea kituo hicho na kutoa zawadi na kucheza na watoto hao mwishoni mwa wiki.
Mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto wenye mazingira magumu cha Sadeline kilichopo Mbezi Juu wilayani Kinondoni,Benedicto Mutayoba akipokea zawadi kutoka kwa mfanyakazi wa kampuni ya Aggrey&Clifford,Martin Kirangu wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipotembelea kituo hicho na kutoa zawadi kwa watoto na kucheza nao mwishoni mwa wiki,aliyembeba ni mama wa mtoto huyo,Grace Thomas. Mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto wenye mazingira magumu cha Sadeline kilichopo Mbezi Juu wilayani Kinondoni,Maulid Rajab akipokea zawadi kutoka kwa mfanyakazi wa kampuni ya Aggrey&Clifford,Ndeshi Rajab
Mfanyakazi wa kampuni ya Aggrey&Clifford,Nia van Aswegen (kulia) akiwapatia zawadi watoto Mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto wenye mazingira magumu cha Sadeline Mfanyakazi wa kampuni ya Aggrey& Clifford, John Alexander akimkabidhi msaada wa mfuko wa vyakula mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha Sadeline. Wafanyakazi wa Aggrey&Clifford wakiwa wamewabeba baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Sadeline
Mfanyakazi wa Aggrey&Clifford,Nadah Dhiyebi akicheza na watoto wa kituo cha Sadeline Aggrey&Clifford yasaidia watoto wenye mazingira magumu --- Kampuni ya matangazo na ukuzaji wa masoko ya Aggrey&Clifford mwishoni mwa wiki imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto wenye mazingira magumu kituo cha Sadeline kata ya Mbezi Juu ambapo pia baadhi ya wafanyakazi wake walishiriki kucheza na watoto hao kwa ajili ya kuwapatia faraja katika msimu huu wa sikukuu. Akiongea wakati wa hafla hiyo Mkurugenzi wa kitengo cha Matangazo ya Biashara wa Aggrey&Clifford,Oliver Mutere, alisema kuwa msaada huo wa nguo na chakula na vifaa vya kusomea ni kwa ajili ya kuwapatia faraja watoto hao wanaoishi katika mazingira magumu. “Moja ya sera ya kampuni yetu ni kusaidia shughuli za kijamii ikiwemo kuunga mkono jitihada za serikali za kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo kwenye jamii ndio maana katika kipindi hiki tumeonelea kuna umuhimu wa kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika kata hii ya Mbezi Juu”.Alisema. Mutere alisema mbali na kutoa msaada wafanyakazi wa Aggrey&Clifford wamekuwa na utaratibu wa kujitoa na kutoa muda wao kwa ajili ya kusaidia kazi za kijamii “Kutokana na sera hii baadhi ya zawadi hizi zilizotolewa zimetokana na michango ya wafanyakazi”. Mratibu wa kituo cha watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu cha Sadeline ,Sarah Kitainda,alishukuru kwa msaada huo ambao alidai kuwa umeleta faraja kwa watoto hao hususani katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu ya Krismas na mwaka mpya. “Kwa niaba ya kituo hiki natoa shukrani kwa kampuni ya Aggrey&Clifford kwa kuwakumbuka watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wa kata hii ya Mbezi na ni matumaini yangu kuwa mtazidi kushirikiana nasi kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazotukabili kuwalea watoto hawa katika siku za usoni.
Post a Comment