Moja
ya eneo la lililotumiwa na kampuni ya Polyphon Film ya nchini Ujerumani
ikirekodi Filamu inayozungumzia maisha kwa ujumla eneo la Kogatende
ndani ya Hifadhi ya taifa ya Serengeti mkoa wa Mara na inatarajiwa
kukuza utalii .
Mkurugenzi
wa kampuni ya Hatari Lodge ya jijini Arusha(kushoto)Gabriel na Meneja
Uzalishaji wa kampuni ya Polyphon Film,Manuel Shrouder wakiwa eneo la
kutengeneza filamu hiyo itakayooneshwa kwenye kituo maarufu cha Runinga
cha ZDF nchini Ujerumani na kutazamwa na zaidi ya watu 10 milioni katika
nchi tatu zikiwemo Austria na Uswizi.
Meneja
Uzalishaji wa kampuni ya Polyphon Film,Manuel
Shrouderk(kulia)akisalimiana na Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa
shirika la Hifadhi za Taifa(Tanapa)Ndg Ibrahim Mussa(katikati)
anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Hatari Lodge ya jijini
Arusha,Gabriel.
Mratibu
wa Uzalishaji wa kampuni ya Polyphon Film,Mona Lessink akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu filamu hiyo itayoanza kurushwa katika kipindi
cha Pasaka mwaka 2017,kushoto ni Meneja Uhusiano wa Tanapa,Pascal
shulutete akifatilia kwa karibu.
Sehemu ya magari yaliyobeba vifaa vya kutengeneza filamu hiyo ambayo imegharimu kiasi cha Euro 1.7 milioni
Wataalamu wa kampuni hiyo wakiwa eneo la kutengeneza filamu ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti
Askari wanyamapori wa Hifadhi ya Taifa Serengeti wakiimarisha ulinzi kwa wageni hao
Katika
kuboresha filamu hiyo upigaji wa picha kwa kutumia ndege ndogo ili
kuonyesha madhari ya Hifadhi ya Taifa Serengeti ulifanyika chini ya
usimamizi wa Tanapa.
Post a Comment