Samwel Mwakalobo Bwanaharusi ambaye ameingia mitini muda mchache kabla kuingia kanisani kufunga ndoa katika kanisa la K.K.K.T Isanga jijini Mbeya. |
Na JamiiMojaBlog ,FahariNews
Mwisho wa mwaka 2016 huenda ukamaliza na kituko cha aina yake
katika Mitaa ya Isanga Jijini Mbeya Mkoa
wa Mbeya mara baada ya bwanaharusi
kuingia mitini masaa machache kabla ya kufunga ndoa.
Tukio hilo la aina yake limeibua maswali mengi kwa ndugu
jamaa na marafiki ambao walikuwa tayari kwa maandalizi ya kuhudhuria harusi
hiyo kuanzia kanisani hadi ukumbini.
Imeelezwa kuwa mipango yote ya harusi ilifanyika kwa pande
zote mbili kushiriki kwa kufuata
taratibu zote zinazotakiwa kufuatwa hadi hatua ya mwisho ya kuingia kanisani
ambapo kama kawaida ndugu jamaa wote walihudhuria kanisani kwa lengo la
kushuhudia tukio hilo .
Tukio rasmi lilianza majira ya saa 7 mchana katika kanisa la
K.K.K.T Usharika wa Isanga jijini Mbeya
Desemba 16 ambapo kama kawaida
Bibi harusi akiongozana na wapambe wake akifuata na msafara wa magari zaidi ya
manne akitokea Saloon na kuingia
kanisani hapo.
Baada ya bibi harusi kuingia kanisani tayari kwa kufunga ndoa
hiyo taarifa zilianza kuenea kuwa
bwanaharusi hayupo kanisani hapo na hajulikani mahali alipo.
Kadri muda ulivyozidi kwenda bila bwana harusi kufika
kanisani hapo baadhi ya Ndugu, jamaa na watu
waliohudhuria harusi hiyo walianza kuhoji ambapo kwa muda huo yalipita zaidi ya
masaa 4 bila chochote kuendelea kanisani hapo.
Kadi ya mualiko kwa ajiliya sherehe |
Bibi harusi Given Mgaya Mkazi wa Isanga jijini Mbeya |
Akielezea mkasa huo Mchungaji kanisa la K.K.K.T Usharika wa Isanga Ndugu Andagile Mwakijungu amesema jambo hilo
amelipokea kwa masikitiko makubwa kwani halijawahi tokea toka ameanza
kutoa huduma kanisani hapo.
Amesema taratibu zote za kufungwa ndoa hiyo zilifanyika na
Jana Desemba 15 majira ya saa 10 jioni wahusika wote Samwel Mwakalobo ambaye
ni bwana harusi na Given Mgaya ambaye ni bibi harusi walifika nyumbani kwa baba
mchungaji na kuafikiana kuwa harusi hiyo
ifanyike leo majira ya saa 7 mchana Desemba 16 kanisani hapo hivyo kitendo cha bwanahurusi kutofika bila sababu yoyote yeye mwenyewe imestua hasa kutokana na mipango ilivyokuwa imepangwa vizuri .
Amesema jambo hilo limetokea wakati yeye akiendelea kufanya
maandalizi ya kusubiri kutoa huduma ya
kufunga ndoa kati ya wawili hao .
Amesema wakati akiendelea kusubiri ili kufungisha ndoa hiyo
walitokea ndugu upande wa mume ambao waliomba msaada kwa mchungaji ili
awasaidie kumtafuta kijana wao ambaye ni bwanaharusi kwa njia yoyote ili kufaham chanzo kilichopelekea
kushindwa kufika kanisani hapo bila kutoa sababu zozote.
Amesema alichukua jukumu la kumtafuta kijana huyo ambapo
alifanikiwa kumpata na kuzungumza nae ambapo kijana huyo alimueleza kuwa
anatatizo na baadae angefika kwa mchungaji ili kumueleza.
“Baada ya
wazazi kufika na kunieleza kuwa nisaidie kumtafuta kijana wao nilichukua jukumu
hilo na nilifanya hivyo na nilifanikiwa kumpata lakini alicho nijibu nikuwa
mchungaji ninatatizo hivyo nitafika ofisini kwako kukueleza na kwa sasa nipo
njiani nikitokea Tunduma ”Amesema
Mchungaji amesema kuwa wakati wanaendelea na majadiliano ya
nini kifanyike ghafla walipata ujumbe
kutoka kwa mpambe wa bwanaharusi ambao ulitumwa na bwanahaurusi mwenyewe ukieleza
kuwa asingeweza kufika ili kufunga ndoa
hiyo bila kueleza sababu yoyote.
Gari lililombeba Bibi harusi |
Kufuatia tukio la bwanaharusi kuingia mitini huku jitihada za
kumpata kushindiana Mchungaji huyo aliamua kusitisha zoezi la ufungaji wa ndoa
hiyo.
“Nimejaribu
kutafuta suluhisho la ndoa hii ili ifungwe licha ya kuchelewa lakini mpaka sasa
hakuna dalili zozote kuwa ndoa hii itafungwa kwani bwanaharusi hajulikani alipo
hivyo nimesitisha ndoa hii na niwaombee ndugu mkafanye jitihada zenu kumtafuta
kijana huyu na mfikie muafaka kwa pande zote mbili ”Alisema Mchungaji.
Amesema taratibu za
ndoa zinataka siku 21 ndoa ifungwe hivyo yeye kama mchungaji kisheria ndiye
mdhamini na mtangazaji wa kisheria kwa suala la ndoa ya mwaka 71 ambayo inampa
mamlaka ya kueleza kwanini ndoa haikufungwa
kwa siku 21 kwa mujibu wa sheria.
Bibi harusi atolewa kanisani akiwa amevuliwa shera …………………
Katika kile ambacho kilisubiliwa kwa hamu na ndugu na jamaa
kuona hitimisho la ndoa hiyo ambapo bibi
harusi aliingizwa katika gari maalumu bila kuvalishwa shera pamoja na kufunikwa
kanga na kuondoka kanisani hapo majira ya saa 10 jioni wakielekea pasipo
julikana huku baadhi ya ndugu wakionesha majonzi na wengine kutokwa na machozi kwa
kutoa amni kile kilichotokea .
Waliochanga kwa ajili ya sherehe ya usiku……………
Mara baada ya sinema hiyo kukamilika kanisani ndugu na jamaa
waliochanga pesa zao kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya usiku walianza kueleza
kuwa watafika ukumbini kama kawaida na kula chakula na kunywa ili kufidia pesa
yao.
Sherehe hiyo ilipangwa kufanyika katika Ukumbi wa Mkapa Hall
jijini Mbeya na kuhudhuriwa na watu zaidi ya mia tatu ambapokila kwa michango
wanakamati ilikuwa laki moja na wengine shilingi elfu 70.
Mwisho.
Post a Comment