VIJANA
kutoka Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Wilaya ya Arusha Mjini
wakiungwa mkonoba baadhiya wananchi wengine wamefanya zoezi la
kuchangia damu kwa ajili ya kusaidia hospitali yaMt Meru inayokabiliwa
na upungufu mkubwa wa damu hali inayochangia ongezeko la vifo hasa akina
mama wakati wa kujifungua.
Akizungumza
jana katika katika Hopsitali ya Mt Meru, mratibu wa zoezi hilo kwa
upande wa wachagiaji, Katibu wa BAVICHA Wilaya ya Arusha Mjini ambaye
pia ni Diwani wa Kata ya Levolosi Mh Glory Kaaya alisema zoezi hilo
limefanyika maalum kama tukio la kuaga mwaka huu wa 2016 kwa
kuwahamsiaha vijana wenzake na wanajamii wengine kujitolea kuchangia na
kusaidia kupunguza upungufu wa damu katika hospitali ya Mt Meruwakiamini
mchango wao utasaidia kuokoa maisha ya watu wengi.
Miongoni
mwa watu mashuhuri waliojitokeza kuunga mkono zoezi hilo ni pamoja na
Mbunge wa Simanjiro Mh James Olemiya, Naibu Meya Jiji la Arusha Viola
Likindikoki pamoja na baadhi ya madiwani wa Baraza la Halmashauri ya
Jiji la Arusha akiwemo Ddiwani Ephata Nanyaro wa Kata ya Levolosi na
Rick Moiro wa Kata ya Moshono.
Sehemu ya damu ambayo ilipatikana jana itakayowafaa wahitaji na kusaidia tatizo la upungufu wa damu |
Mwenyekiti waBAVICHA Arusha Mjini ambaye pia ni Katibu wa Mbunge wa Arusha Mjini Innocent J Kisanyage akijaza fomu maalumu kablaya kutolewa damu |
Mtaalamu wa afya akiendelea nahuduma ya uchangiaji damu |
Diwani wa Kata ya Levolosi Mh Ephata Nanyaro akiendelea kutolewa damu |
PICHA NAMAELEZO: ARUSHA255 BLOG
Post a Comment