Nigeria imekamata magunia 102 ya
''mchele wa plastiki'' yaliyokuwa yanaingizwa nchini humo na
wafanyabiashara haramu ambao walitaka kuuza katika msimu huu wa sherehe,
kulingana na afisa wa forodha katika mji mkuu wa nchi hiyo , Lagos.
Uchunguzi
wa awali ulibaini kuwa mchele huo ulikuwa ni wa "plastiki'' ,baada ya
kuuchemshwa, na kuoneka kuwa mkubwa zaidi ya mchele wa kawaida na ni
Mungu tu anajua ni nini ambacho kingetokea kama ungeliwa na binadamu ",
Haruna Mamudu aliongeza katika kauli yake juu ya tukio hilo.
Aliwawaonya
wahujumu wa uchumi ambao wanangalia kipindi hiki cha sherehe kama
njia za kupata mapato kwa udanganyifu kuwa watakabiliwa na mkono wa
sheria.
Bwana Mamudu hakuelezea ni vipi mchele huo wa plastiki ulitengenezwa lakini ulikua na nembo iliyoandikwa "Best Tomato Rice".
Uchunguzi
unaendelea kutambua ni kiwango gani cha mchele huo kimekuwa kikiuzwa
na ni vipi unaweza kuondolewa sokoni ili kulinda afya za raia wa Nigeria
waliokwisha utumia na kuwapeleka wahusika wa biashara hiyo haramu
mbele ya sheria".
Nchini Uchina, kuliwahi kuwa na sakata ya
chakula mwaka jana baada ya kubainika kuwa kuwepo kwa mchele
uliotengenezwa kwa plastiki.
Post a Comment