Jaji mmoja nchini Zimbawe amemwaagiza mke wa rais Robert Mugabe,
Grace Mugabe, kurudisha nyumba tatu alizompokonya mfanyabiashara nmoja
raia wa Lebanon, kufuatia zabuni ya pete ya almasi ya gharama ya dola
milioni 1.35.
Kulingana na kesi iliyowasilishwa na mfanyabiashara
huyo, Bi Mugabe alitaka kurudishiwa pesa baada ya pete hiyo ya almasi
iliyonunuliwa mjini Dubai. ilipowasilishwa kwake baada ya kutengenezwa
na mtu tofauti
Wakati Jamal Ahmed alishindwa kulipa pesa hizo kwa akaunti mjini
Dubai, na licha ya yeye kusema kuwa pesa hizo zilitumwa kupitia kwa
benki moja ya Zimbabwe, Bi Mugabe alichukua kwa nguvu nyumba zake tatu
mwezi Oktoba.
Jaji Clement Phiri alisema kuwa Bi Mugabe pia ni
lazima ahakikishe kuwa wafanyakazi wote waliokuwa wakihudumu kwenye
nyumba hizo wamerudishwa kazini.
Pete hiyo ilikuwa ni kama zawadi kwa mke wa rais Mugabe, Bi Grace, kuadhimisha miaka 20 ya ndoa.BBC
.
Post a Comment