Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji Mstaafu Damiani Lubuva (kushoto)
akiongoza kikao cha Wajumbe wa Tume na Sekretarieti cha Usaili wa
Waratibu na Wasimamizi Uchaguzi mdogo katika jimbo la Dimani, Zanzibar
utakaofanyika Januari 22, 2017.
Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhan
(katikati) akitoa ufafanuzi kwa Wajumbe wa Tume na Sekretarieti ya Tume
wakati wa kikao cha Usaili wa Waratibu na Wasimamizi wa Uchaguzi mdogo
katika jimbo la Dimani Zanzibar. Kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa
ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damiani Lubuva na Kulia ni Mjumbe wa Tume Mhe.
Mchanga Mjata.
Baadhi
ya Wajumbe wa Seckretarieti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
wakifuatilia kwa makini zoezi la Usaili wa kuwapata Waratibu na
Wasimamizi wa Uchaguzi mdogo katika jimbo la Dimani Zanzibar leo.
Wajumbe
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakipitia vyeti na nyaraka mbalimbali
wakiongozwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu
Damiani Lubuva wakati wa Usaili wa nafasi ya Waratibu na Wasimamizi wa
Uchaguzi mdogo katika jimbo la Dimani utakaofanyika Januari, 22, 2017.
Mmoja
wa washiriki wa Usaili katika nafasi ya Mratibu wa Mkoa katika Uchaguzi
mdogo wa Jimbo la Dimani Bw. Salum Juma Mgunya akijieleza wakati wa
Usaili mbele ya Wajumbe wa Tume na Sekretarieti ya Tume ya Taifa ya
Uchaguzi leo mjini Zanzibar.
Mmoja
wa washiriki wa Usaili katika nafasi ya Msimamizi wa Uchaguzi katika
Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani Bi. Fatma Gharib Haji akijieleza
wakati wa Usaili mbele ya Wajumbe wa Tume na Sekretarieti ya Tume ya
Taifa ya Uchaguzi leo mjini
Wajumbe
wa Sekretarieti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakifuatilia Usaili wa
Wasimamizi na Waratibu wa Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani Zanzibar. Picha na Aron Msigwa – NEC, Zanzibar.
Post a Comment