Makamba
amesema hayo wakati wa Kongamano la wadau wa Nishati ya umeme
walipokutana kuzungumzia matumizi ya Nishati ya umeme inayozalishwa kwa
njia ya upepo itakayounganishwa kwenye gridi ya taifa na mfumo huo
utawasaidia wananchi wa Singida .
"Kwa
kuwa umeme huo utazalishwa kwenye maeneo ya vijijini, wananchi
wanatakiwa kupata umeme kwa bei rahisi kulingana na uchumi wao na sio
kuuziwa umeme kwa bei juu, na zaidi Wizara yake inapenda kuweka wazi
kuwa huu mradi una faida kubwa sana kulingana na mfumo wa nchi
ulivyo,"amesema Makamba.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya kuzalisha umeme wa upepo Afrika Mashariki Six
Telecoms, Rashid Shamte amessema kuwa mfumo huu wa gridi ndogondogo una
faida kubwa sana kwa wananchi kwani asilimia kubwa kulingana na ripoti
ya benki ya dunia wananunua umeme wa bei nafuu kwahiyo serikali
imekubaliana na kampuni yetu na imeweza kukubali kuwa mradi huu una
tija na utasimamiwa na serikali yenyewe kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa
Singida pamoja na Halmashauri.
Shamte
ameendelea na kusema, kwa Phase ya kwanza watatoa umeme megawati 100 na
itaendelea mpaka kufika megawati 300 na wataunganisha kwenye gridi ya
taifa, na huu mradi utakuwa na faida kwa wananchi pamoja na wale
watakaotolewa kwenye maeneo yao watafaidika kwa kulipa stahiki zao.
Kwa
upande wa Wizara ya Nishati na Madini, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo
amewataka wawekezaji hao kuuza umeme kwa bei rahisi kwani mara nyingi
mipango ya serikali imekuwa haiendani na mikakati ya wawekezaji kwahiyo
wanategemea kuona kuwa mradi huu uwe nafuu ya wananchi wa vijijini
kupata umeme kwa bei rahisi.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano Mheshimiwa
January Makamba akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa umeme kujadili
mkakati ya kuzalisha nishati ya Umeme kwa njia ya Upepo leo katika
ukumbi wa Hotel ya Hyatt Jijini Dar
Mkurugenzi
Mtendaji Six Telecoms, Rashid Shamte (wa kwanza kushoto) akiwa kwenye
kongamano la wadau wa umeme wenye lengo la kuzalisha umeme wa nguvu ya
Upepo wenye lengo la kuanza kuzalisha umeme katika mkoa wa Singida.
Baadhi ya wadau wakiwa kwenye kongamno la wadau wa umeme
Mkurugenzi Mtendaji Six Telecoms, Rashid Shamte akizungumzia uzalishaji wa umeme kwa njia ya upepo utakaosimamiwa na Kampuni ya kuzalisha umeme huo ya Afrika Masharikana awamu ya kwanza itaanzia mkoani Singida.
Alex Moulds kutoka Energy Net Limited akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuzalisha umeme wa Upepo
Post a Comment