Mwigizaji mashuhuri Mmarekani Zsa Zsa Gabor amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 99.
Wengi wanasema nafasi kuu zaidi aliyoiigiza maishani ni kujiigiza mwenyewe na kugeuza maisha yake kuwa kama filamu moja ndefu.
Ingawa aliigiza kwenye zaidi ya filamu 70, ndoa zake nyingi na maisha yake ya kifahari ndivyo vilivyompatia sifa nyingi.
Alipokuwa
katika jamii ya waigizaji Hollywood, alidumisha sifa fulani za kipekee
na kujionyesha kama mtu wa familia tajiri yenye mamlaka Hungary.
Alizungumza lugha saba, lakini licha ya kuishi California zaidi ya nusu karne, hakuwahi kupoteza lafudhi yake.
Alizaliwa
Sari Gabor mjini Budapest tarehe 6 Februari 1917 lakini mara moja
alipewa jina la utani Zsa Zsa na watu wa familia yake.
Alikuwa binti wa pili wa baba mwanajeshi na mama tajiri wa vito.
Alitaka
awali kuwa daktari wa upasuaji wa mifugo lakini mamake hakutaka hilo.
Kutokana na urembo wake, alielekea njia tofauti - mitindo na uigizaji.
Mamake
alikuwa Myahudi, ingawa binti zake watatu walikuwa waumini wa kanisa
Katoliki. Huo ulikuwa uamuzi wa busara ikizingatiwa kwamba Hungary
ilikuwa inatawaliwa na Miklos Horthy aliyekuwa na urafiki na Adolf
Hitler wa Ujerumani.
Post a Comment