Diamond akikabidhiwa bendera ya Taifa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye
Kumekuwa
na sitofamu katika mitandao ya kijamii kuhusu ni nani anastahili
kukabidhiwa bendera ya Taifa ili kuwakilisha nchi, baada ya Diamond
Platnumz kukabidhiwa bendera ya Taifa jana na Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye kwajili ya show yake
ya kutumbuiza ufunguzi wa michuano ya Afcon 2017 inayofanyikia nchini
Gabon weekend hii.
Mashabiki
wengi katika mitandao hiyo wamekuwa wakizozana bila kupata jibu kwamba
ni kwanini Diamond alikabidhiwa bendera hiyo kwa ajili ya kuwakilisha
Tanzania wakati anaenda kufanya show yake binafsi.
Akiongea
Alhamisi hii kuhusu suala hilo Katibu mkuu wa na Baraza la Sanaa la
Taifa (Basata) Godfrey Mngereza amesema bendera ya Taifa anaweza kupewa
mtu yeyote ambaye anaenda nje ya nchi, na safari yake ina manufaa kwa
taifa lake.
“Suala
wa Waziri Nape ambaye ndiye Waziri mwenye dhamana ndani ya Wazira wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kumkabidhi Diamond bendera ya Taifa
ni jambo zuri kwa sababu ingawa Diamond anakwenda kufanya show yake
lakini tukumbuke yule ni mtanzania pekee pale ambaye anakwenda
kuliwakilisha Taifa lake kwa show yake mbele ya maelfu ya watu Afrika
nzima, jina lake linatambulika pale lakini wao wanamtambua yule kama
mtanzania na hata akifanya vizuri sifa zinaenda kwa yeye pamoja na Taifa
lake,” alisema Nngereza.
Pia
Nngereza alidai mtanzania yeyote anaweza kukabidhiwa bendera ya katifa
kama anaenda kufanya tukio lolote ambalo linaweza kuipatia sifa nchi
yake kwa namna yoyote.
“Mtu
yoyote ambaye anaenda nje ya nchi kwa ajili ya matamasha makubwa au
kama kuna namna ambavyo anaenda kufanya kitu ambacho kimpatia yeye faida
pamoja na Taifa lake anaweza kukabidhiwa bendera, awe mtanzania tu. Kwa
hiyo hata ukiwa mtangazaji, mchezaji, vikundi vya ngoma na sanaa
mbalimbali wanaweza kukabidhiwa bendera kama wakihiitaji kwa sababu kuna
wengine hawatoi taarifa kuhusu matukio yao lakini kama ukitoa taarifa
na mamlaka ikaona kuna umuhimu wa kufanya tunafanya hivyo kwa sababu ni
kwa ajili ya taifa letu,”
Post a Comment