Mshambuliaji wa TP
Mazembe na timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Thomas Ulimwengu amejiunga
na timu ya Ligi Daraja la Kwanza Nchini Sweden inaitwa Athletic
Football Club Eskilstuna kwa mkataba miaka miwili
Baada ya mkataba wake
ulimalizika, Mabingwa wa kombe la Shirikisho barani Afrika TP Mazembe
Ulimwengu hakutaka kuongeza mkataba mwingine kwani mawazo yake yalikuwa
ni kumfuata rafiki yake Mbwana Samatta anayekipiga KRC Genk ya Ubelgiji
.
Akizungumza na
Ulimwengu alisema: “Kweli nimesajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili
kuitumikia timu hiyo ambacho nitajiunga nayo hivi karibuni.
“Kwa sasa
nashughulikia mambo ya visa kuanzia wiki ijayo nitaenda nimeshajiunga
na timu ya Athletic Football Club Eskilstuna ya Sweden.”
Ligi hiyo ya daraja la Kwanza inashirikisha timu kumi na nne na inatarajia kutumia vumbi April kumi na nne mwaka huu.
Post a Comment